in , , ,

KAMATI YAPITIA USAJILI, NGASA KUCHEZEA YANGA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya
kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini
kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa
na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh.
milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo
kwa Simba.

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya
Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha
kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha
hizo.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa
wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe
zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza
hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya
kufanya kazi nchini (work permits).

Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti
za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na
kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

20130817-081421.jpg

*UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 27*

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa
kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za
Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20
mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.

Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20
mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi
ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano
Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.

Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa mabadiliko
hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa
uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika
mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.

Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18
mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na
inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

KAMATI YA UCHAGUZI KUJADILI SIMBA, YANGA

Pazia Ligi Kuu England lafunguliwa