in , ,

KAGAME CUP KUENDELEA 21/07/2015

Yanga

Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam, kesho jumanne itaingia katika siku ya nne kwa kuwakutanisha Azam FC dhidi ya Malakia kutoka Sudani Kusini, mchezo utakochezwa katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10 kamili jioni.

Mchezo wa kwanza utakaoanza majira ya saa 8 kamili mchana uwanja wa Taifa utazikutanisha timu za Al Shandy ya Sudan dhidi ya LLB ya Burundi, huku uwanja wa Karume majira ya saa 10 kamili jioni Heegan FC ya Somalia wataonyeshana ubavu dhidi ya APR kutoka Rwanda.

Jumatano kutakua na michezo mitatu ambapo mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa utawakutanisha Khartoum ya Sudan dhidi ya KMKM ya Zanzibar saa 8 mchana, huku uwanja wa Karume saa 10 jioni KCCA ya Uganda watawakaribisha Adama City kutoka Ethiopia.

Katika uwanja wa Taifa jumatano saa 10 jioni, Telecom ya Djibout watakua wenyeji wa Yanga SC ambayo kocha wake mkuu Hans Van Der Pluijm ameahidi kupata ushindi katika mchezo huo.

Hans amesema mchezo wa ufunguzi dhidi ya Gor Mahia walipoteza kutokana na kucheza pungufu kwa takribani dakika 60, hivyo anawaanda vijana wake kufanya vizuri siku ya jumatano na kuwapa furaha wanachama na wapenzi wa Yanga SC.

KHATROUM, GOR MAHIA ZASHINDA
Mabingwa mara tano wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, leo imeshinda mchezo wake wa pili mfululizo baada ya kuichapa KMKM ya Visiwani Zanzibar kwa mabao 3-1.

Mabao ya Gor Mahia yalifungwa na mshambuliaji Meddy Kagere bao moja, Michael Olunga aliyefunga mabao 2, huku bao la kufutia machozi la KMKM likifungwa na Matheo Anthony.

Katika mchezo wa awali uliochezwa saa 8 mchana, Khartoum ya Sudan iliichapa timu ya Telecom ya Djibout kwa mabao 5- 0, mabao ya Khartoum yalifungwa na Wagdi Abdallah, Ousmaila Baba, Murwan Abdallah, na Salah Bilal aliyefunga mabao mawili.

Kwa matokeo hayo ya leo Gor Mahia wamefikisha pointi 6, wakifuatiwa na Khartoum yenye pointi tatu sawa na KMKM wakipishana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Wakati huo huo kesho siku ya jumanne waandishi wa habari walioomba vitambulisho vya kufanyia kazi (Accreditation) wanaombwa kufika ofisi za TFF zilizopo Karume kuchukua vitambulisho vyao.

Waandishi mnaombwa kuchukua vitambulisho hivyo kuanzia saa 5 kamili asubuhi mpaka saa 6 kamili mchana, kwani vitambulisho vya muda vilivyotolewa havitatumika tena.

Kuanzia michezo ya kesho jumanne kila mwandishi atapaswa kutumia kitambulisho kilichotolewa maalum kwa ajili ya michuano hiyo kuingilia uwanjani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Arsenal wampigia hesabu Dzeko

UARGENTINA NI TATIZO KWA MESSI