in , ,

Jürgen Klopp: KUNA HAJA YA KUZUNGUMZA NA NAFSI

England ina historia kubwa sana duniani. Pamoja na kwamba hawa watu
ndiyo walikuwa wa kwanza kugundua teknolojia duniani na kuifanya
England kuwa sehemu kubwa ya soko la biashara duniani enzi hizo, pia
ndiyo nchi iliyokuwa na Makoloni mengi sehemu mbalimbali za dunia.

Walijivunia kuwa na makoloni mengi ambayo yaliwasaidia kwa kiasi
kikubwa kupata Malighafi za viwanda vyao.

England ikawa nchi yenye viwanda vingi, utajiri wake ukawa unaongezeka
kwa kasi. Waingereza wakawa wanajivunia kwa kiasi kikubwa na nchi yao.

Kila Mwingereza alitembea kifua mbele akijivunia nchi yake, walitawala
kila sekta. Wakaonekana wao ndiyo bora.

Hata mchezo wa mpira wa miguu ulianzia kwao, wakaishi kwa kuamini wao
wamezaliwa na mpira. Wamekuwa na mpira na wanaujua mpira kwa sababu
wanauishi mpira.

Wakatengeneza timu nyingi ambazo zitawafanya wao wajivunie kwa
kutembea kifua mbele kwa kuamini hizo timu ni nembo ya nchi.

Moja ya timu hizo ni Liverpool. Timu yenye mashabiki wengi nchini
England. Timu yenye historia kubwa England na ambayo watu wengi
hujivunia nayo kila uchwao.

Utawaambia nini Waingereza juu ya Liverpool wasikuelewe? Hii ni moja
ya nembo yao.

Nembo ambayo inahangaika kwa miaka 20+ bila kombe la ligi kuu ya England.

Nembo ambayo ina kiu kali ya mafanikio ambayo hawajayapata kwa muda mrefu.

Na matamanio ya wengi ni kuiona Liverpool ikifika sehemu ambayo ni
kubwa zaidi ambayo wameshindwa kufika kwa muda mrefu.

Kila shabiki wa Liverpool anamatamanio ya kuiona Liverpool ikishinda
kombe la ligi kuu lakini wanasubiri ni nani ambaye atakuja kuondoa kiu
ya matamanio ya mashabiki wa Liverpool.

Klop aliaminiwa, imani ambayo iliwafanya wengi wa mashabiki wa
Liverpool siku za neema kwao zimewadia.

Klop ambaye alifanya vizuri kabla na Borrusia Dortmund ya Ujerumani ,
wengi waliamini mafanikio hayo yatakuja kwenye klabu ya Liverpool.

Alifanikiwa kushinda kombe la Ujerumani, kombe la Bundesliga na kufika
fainali ya UEFA akiwa na kikosi cha gharama ndogo ukilinganisha na
timu zingine.

Imani hii ya kujenga timu imara kupitia wachezaji wasio na gharama
kubwa iliwafanya wengi waamini ana uwezo mkubwa wa kufanya maajabu
katika timu ya Liverpool.

Maisha ya kusubiri siku zenye neema yalianza kwa mashabiki wa
Liverpool kuzisubiri hizo siku kwa shauku kubwa.

Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda giza zito linatanda mbele yao,
mwanga wa matumaini unazidi kufifia kadri siku zinavyozidi.

Timu imekuwa na matatizo sehemu ya ulinzi, imekuwa timu ambayo
ikiruhusu magoli mengi ambayo ni ya kizembe. Magoli ambayo ni vigumu
kwa timu yenye beki imara kuruhusu aina hiyo ya magoli.

Pamoja na kwamba beki ya Liverpool inaruhusu magoli mengi ya uzembe,
pia eneo lao la kiungo linaruhusu sana mashambulizi kwa mabeki.

Hakuna kiungo wa kati wa asili wa kujilinda, viungo wote wa kati wa
Liverpool asilimia kubwa wana akili ya kushambulia na ndogo ya
kujiuzuia.

Hii ndiyo aina ya soka ambayo Klop anaitaka, anataka timu ishambulie
kwa nguvu na kasi huku ikicheza soka la kuvutia.

Ni ngumu hata kwake yeye kuamua kuweka angalau kiungo ambaye w
ana asilimia kubwa ya akili ya kuzuia katika eneo la kati ili kiungo
huyo awe ana kaa mbele ya mabeki wanne kuwahakikishia ulinzi wao.

Hii itakuwa ngumu kwa Klop kwa sababu itapunguza kasi ya kwake
kuanzisha mashambulizi.

Pamoja na kwamba Liverpool inacheza mpira wenye kasi , pia
inatengeneza nafasi nyingi za magoli.

Ndiyo timu pekee ambayo inategeneza nafasi nyingi za magoli lakini
haizitumii ipasavyo.

Hapo kosa siyo la Klop, moja ya jukumu la kocha ni kuhakikisha timu
inatengeneza nafasi nyingi za magoli na kazi ya kufunga inakuwa sanaa
ya mchezaji.

Kocha hafundishi jinsi ya kufunga, anafundisha jinsi ya kutengeneza
nafasi za kufunga. Kufunga kunabaki kuwa sanaa ya mchezaji husika.

Hivo basi kama mchezaji anashindwa kubadirisha nafasi za kufunga kuwa
magoli basi hapo shida inakuwa timu haina mtu wa kufunga magoli.

Ndipo hapo kunapokuja kwenye ukweli kuwa Liverpool haina mfungaji
halisi, mshambuliaji halisi wa kati ambaye anaweza kuzitumia nafasi
nyingi za kufunga kuwa magoli.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

CONTE ALIJIANGAMIZA MWENYEWE?

Tanzania Sports

MKUDE , BENCHI LINAMUONDOLEA KILA KITU