in ,

JKT maarufu kwa timu za netiboli sasa wataka ubingwa wa soka

KWA miongo kadhaa Timu za Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi zimekuwa maarufu kwa mchezo wa mpira wa pete (Netball).
Timu hizo zimekuwa zikitamba na kuwa mabingwa wa Tanzania bara   mara zote wakati mara kadhaa kwa upande wa Afrika Mashariki.

Miongoni mwa timu hizo za netiboli ni  Jeshi Stars na  Mbweni JKT  ambazo kwa kipindi kirefu zimekuwa zikichuana vikali katika kubadilishana ubingwa.
Lakini wakati mambo yakienda vizuri kwa upande wa timu za netiboli,  majeshi hayo yalikuwa kimya bila ya kuwa na timu yoyote ya maana katika masuala ya mpira wa miguu.
Katika kipindi hicho ni Idara ya Magereza iliyofanikiwa kuwa na Timu ya Prisons iliyokuwa na makao makuu jijini Mbeya ambayo sasa imeporomoka na kuwa katika ligi ya daraja la kwanza.
Nalo polisi, miaka mitano iliyopita liliandaa mkakati wa kuwasaka vijana wanaojua kucheza soka na kufanikiwa kuwa na Timu ya  Polisi Dodoma ambayo mpaka sasa ndiyo inayocheza Ligi kuu ya Tanzania.
Wakati polisi wakifikiria hilo, nalo Jeshi la Kujenga Taifa  bila shaka kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi  liliweka mkakati wa kuandaa timu za soka  ambapo  tatu zilifanikiwa kuingia kwenye ligi kuu.
Mpaka  sasa Jeshi la Kujenga Taifa lina timu tatu za soka ambazo zimeonyesha kuwa moto katika michuano inayoendelea.
Mkuu wa Kikosi cha Ruvu JKT, Kanali  Mbelle ambaye kikosi chake kina timu za Ruvu JKT na Ruvu Shooting anasema  Jeshi  limejipanga kuinua kiwango cha soka Tanzania.
Anasema lilianza kuipandisha  Ruvu JKT , halafu ikafuata Ruvu Shooting na bahati nzuri mwaka huu Oljoro JKT ya Arusha imeingia na mwakani wamejipanga kuzipokea  Mlale JKT  ya Ruvuma na Mgambo JKT  ya Tanga.
Taarifa zaidi zinasema uongozi wa Jeshi umeshatoa maelekezo kuhakikisha Jeshi linakuwa na timu imara ambayo itakuwa Bingwa wa Tanzania na hatimaye kushiriki  michezo ya kimataifa na kuondoa aibu ya kutolewa mapema katika mashindano  ya  kimataifa.
Kwa  kipindi kirefu timu za Yanga na simba zimekuwa zikitolewa katika mechi za awali katika kuwania Klabu Bingwa Afrika .
Mkakati huo unaonekana kuandaliwa vema mwaka huu kwani tayari timu za JKT zimekuwa miongoni mwa timu ngumu  zikiwa na malengo kamili.
Timu ya Ruvu JK, ilianza kwa mbwembwe kwa  kuitandika  Yanga Sports  goli 1-0 ambayo ni kongwe na yenye mashabiki wengi Tanzania. Hadi Jumapili ya Oktoba 2, timu hiyo ilikuwa imecheza mechi nane  ambapo imeshinda mbili kutoka sare sita na haijapoteza mechi yoyote kama ilivyo Simba Sports Club.

Lakini pia OljoroJKT ilikuwa imecheza mechi tisa na kupata ushindi wa mechi nne , sare mechi nne na kupoteza mechi moja tu, huku Ruvu Shooting ikiwa na sare tano kufunga mara mbili na kufungwa mechi moja.
Kufuatia mwenendo huo, kiongozi wa timu ya Azam ambayo ni moja ya timu kali mwaka huu, amekiri wazi kwamba timu za Simba na Yanga siyo tishio kwake kuliko timu za JKT zilivyo.
Ameesema  kwamba timu hizo zinacheza mchezo wa ushindani na siyo rahisi kuzifunga.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Zanzibar Marathon returns to calendar

Kuzomewa kwa timu ya Azam kwenye uwanja wake kuna maana gani?