in , , ,

Jinamizi kwa kipa aliyekula uwanjani

TUME ya Michezo ya Kubahatisha na Chama cha Soka (FA) England wanachunguza iwapo kanuni zilivunjwa kwa golikipa wa akiba wa Sutton, Wayne Shaw kula wakati wa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal.

Shaw aliyekula na kupigwa picha zilizotundikwa mitandaoni na kwenye magazeti, anadaiwa kuhusika kwa namna Fulani kwenye kamari iliyochezwa na wadau, wengi wakisema lazima angekula wakati huo wa mechi.

Kanuni zinakataza wachezaji kushiriki kwa namna yoyote kwenye kamari, na kadhaa wamepata kuadhibiwa kwa kosa hilo. Shaw anakiri kwamba alijua kuna kamari hiyo, lakini anakataa kwamba alikula njama na washiriki ili apate mgawo wa fedha.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 46 alinaswa akila usiku wa Jumatatu kwenye mechi katika dimba la Gander Green Lane, ambapo Arsenal walisonga mbele kwa kuwapiga mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Theo Walcott na Lucas Perez.

Saa 24 baada ya kufanya kitendo hicho, Shaw ameamua kubwaga manyanga kwenye timu hiyo na Mkurugenzi wa Tume ya Michezo ya Kubahatisha,Richard Watson amesema kwamba lazima uadilifu uzingatiwe katika soka na kuachana na mambo ya utani, ndiyo maana wameanzisha uchunguzi kubaini kipi hasa kilitokea.

“Katika uchunguzi huo tutaangalia iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za kamari na kujua iwapo wahusika wana leseni na wanatimiza masharti yote yanayotakiwa na kuzingatia uadilifu kwenye eneo hilo,” anasema.

Msemaji wa FA ameeleza kwamba wanachunguza kuona iwapo kuna kanuni zao zimekiukwa. Shaw anadai kwamba hakuwa amekula chochote tangu asubuhi, hivyo wasaa huo ulipotokea akaamua kula na aliona kama kichekesho kupigwa picha.

Kocha wa Sutton, Paul Doswel anasema kwamba amesikitishwa na matukio hayo, ambapo ndoto yao ya mechi kubwa dhidi ya Arsenal na uwezekano wa kushinda na kuvuka hatua hiyo imegeuka kuwa jinamizi.

Anasema alizungumza kwa simu na Shaw na kwamba kipa huyo alikuwa akilia hata wakafika mahali wakashindwa kuendelea kuzungumza wakakata simu. Ankasema anamsikitikia kwa hali iliyomfika.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KWA HERI GEOFREY BONY NDAJE , NGOJA NILIFUTE CHOZI LANGU

Tanzania Sports

NILICHOKIONA KWENYE MECHI ZA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA ( UEFA)