in , , ,

Itashangaza Arsene Wenger akikosa ubingwa

 

KUNA wakati soka linaleta matumaini na baadaye likaleta maumivu. Arsene Wenger amepitia vizazi vingi vya wanasoka tangu alipokuwa Monaco ya Ufaransa, hadi kumwibua George Opong Weah hadi kuja kuwalea akina Theo Walcott, Aaron Ramsey na kadhalika. Vijana hao wamekuwa chachu ya ushindi wa Arsenal, huku golikipa wapi Petr Cech akidhihirisha bado yu mahiri langoni.

Arsenal ya sasa imeshukwa, halafu inaonekana Wenger amepania sana ubingwa msimu huu, kiasi kwamba najaribu kubashiri labda anaweza kuachia ngazi akitwaa taji hilo kisha akamkabidhi timu hiyo Pep Guardiola. Hili linaweza kupuuzwa lakini ukweli unabaki Pep Guardiola anahusudu sana uchezaji wa Arsenal na utamaduni wake.

Hata hivyo yapo mambo ya kuayaangalia msimu huu. Arsenal imekuwa ikicheza soka maridadi na kiwango cha usakataji kandanda kimeinuka. Tofauti na ilivyo misimu kadhaa iliyopita, kwa sasa Wenger anayo majembe ya kumpa ubingwa. Arsenal imefanikiwa kupata huduma ya Mesut Ozil, Campbell na ubora wa kinda Bellerin umekuwa kwenye kiwango cha juu.

Sababu kubwa inayoweza kuwapatia Ubingwa Arsenal ni aina ya uwajibikaji na maeneo ya wachezaji wake. Aaron Ramsey, Ozil, Oxlade, Giroud, Campbell, Walcott, wote hawa wanaweza kuifunga timu yoyote. Ubora wa timu ni pale unapokuwa wa mzunguko kwmaba wachezaji wanakuwa na uwezo wa kufunga kila wakati.

Akikukosa Walcott basi Ozil anakufunga. Akikukosa Ozil basi Giroud anakufunga ua Campbell. Uwiano wa kupachika mabao kati ya wachezaji hao ni mzuri na umeimarika sana msimu huu. Mabao yao yanachangia kupunguza jukumu la mmoja mmoja na timu mzima.

Safu ya ulinzi kwa kiasi inaonekana kupumzishwa na upachikaji wa mabao. Kwamba Arsenal inakufunga kwanza kiasi cha kuwapa utulivu mabeki wake. Kama washambuliaji wao wasingekuwa wanafunga mabao basi ingekuwa shughuli pevu katika kulinda lango lao.

WAPINZANI WAO:

Msimamo wa EPL, kwa baadhi ya timu
Msimamo wa EPL, kwa baadhi ya timu

Nawatazama wapinzani wao wakubwa Manchester City kuliko Leicester City. Mpira wa Leicester City umekuja kutoka na kiwango cha soka kuporomoka mno. Leicester imenufika na hilo kiasi kwamba wanaonekana ni timu hatari. Jambo jingine Leicester wana bahati ya mtende maana baadhi ya mechi wanazoshinda huwa zinashangaza mno, kwa mfano dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Manchester City wanaweza kuwa kikwazo cha Arsenal katika mbio za ubingwa. Ni timu ambayo inakuja taratibu mno. Na rekodi zinaonyesha wazi wana wastani mzuri wa ushindani

Katika mechi 22 Man City wameshinda mechi 13, wakati Arsenal wameshinda mechi 13. Man City wametoka droo mechi 4, wana pointi 43 moja nyuma ya Arsenal na Leicester City.

Hawa Leicester City wamecheza mechi 22 na kushinda mechi   12, wametoka sare mechi 8 na kufungwa mechi 2 ambapo wana pointi 44. Arsenal wamefungwa mechi 4 ambazo ni moja pungufu ya 5 za Man City.

Leicester City wana wastani mzuri kwa kupoteza mechi 2 dhidi ya Arsenal na Liverpool. Kwa vyovyote vile wastani huo utazibeba Man City na Arsenal kwenye suala la uzoefu wa ligi.

Naziona timu hizi ndiyo washindani wakubwa wa taji la Ligi Kuu England huku Leicester City ikiwa mnufaikaji wa ubovu wa timu za Manchester United, Liverpool na Chelsea.

Timu zote hizo sio tishio kwa Arsenal ambayo ina sababu zote za msingi kuwa mabingwa msimu huu. Tusubiri.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Azam F.C wanambania Farid Mussa?

Tanzania Sports

IS THE SCANDAL OF TENNIS MATCH FIXING RELATED TO US?