in

Ipo nafasi ya Morrison Simba?

Morrison

Nyota wa Yanga Benard Morrison hatokuwepo katika mchezo wa Yanga dhidi ya Singida United baada ya kwenda kusikojulikana .

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa hajajiunga na timu na hajulikani wapi ameenda.

Hii ni ishara kwamba nyota huyu anahitaji kuondoka mazima na taarifa za chini zinasema kuwa kuanzia Julai mosi hautambui mkataba wa Yanga wa miaka miwili ambao unazungunzwa.

Hadi alipofika huenda nyota huyo akaachana na Yanga hasa inaonekana viongozi kuchoka huku wachezaji wenyewe wakiwa hawana hamu naye kabisa.

Yanga wanahitaji kama wakiachana basi waachane kwa faida , timu ipate faida kwa maana asiondoke na fedha zao aache pesa alizopewa za usajili  ndio aondoke.

Mambo yanakuwa magumu kwakuwa tayari yapo katika vifungu vya sheria ndani ya mkataba.

Kama akiondoka sawa ana asipo ondoka sawa sie kazi yetu kuongea pale  palipokuwa na makandokando.

Taarifa zinasema kuwa Simba wanahitaji huduma yake, kabla ya hapo yeye mwenyewe aliwahi kuthibitisha kuwa walimfuata viongozi wa Simba kujaribu kuhitaji huduma yake huku wakimuahidi donge nono la fedha.

Baada ya majanga yote haya kutokea sijui kama Simba watakuwa katika msimamo wao wa kuhitaji huduma yake maana hakuna timu inayotaka matatizo.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alijinasibu kuwa mchezaji akitua Simba atakutana na vifungu vya sheria vitakavyo mbana.

Mara pap!! Morrison amesaini Simba na kupewa jezi namba 33 itakuwaje na kweli ana nafasi yoyote ndani ya timu hiyo ?

Kwa mpira wa bongo ni kweli ana kipaji kizuri kulingana na mahitaji ya ligi ya Tanzania je ni mtu sahihi kwa Simba kutokana na kikosi kilichopo? hili ndio swali kila mmoja anatakiwa ajiulize.

Tuanzie hapa katika safu ya ushambuliaji ya Simba kuna wachezaji wafuatao.

Deo Kanda, Hassan Dilunga, Luís Miquissone, John Bocco, Meddie Kagere na Miraji Athumani.

Kati ya hao ngoja tuwatoe Meddie Kagere na John Bocco ambao mara nyingi wanahudumu  katika eneo la ushambuliaji.

Tubakie  na hao wengine ambao nimewataja, mara nyingi Morrison anacheza kama winga ya pembeni huku akiingia ndani wakati akiwa na mpira.

Hivi kumsajili Morrsion kunaweza kumuweka nje Miquissone ambaye ana kila kitu katika kazi yake kuanzia nidhamu, kasi yake pamoja na ubora wa kufunga magoli?

Unamsajili Morrison wewe kiongozi wa Simba una mpango gani kwa mtu mwenye kipaji kama Miraji Athumani ? achana na Utanzania wake una mpango gani kwa huyu mtu?

Wakati unaendelea kuangalia nafasi ya Morrison bado unawawaza viongozi wa Simba hivi timu imeendelea na imefanya mabadiliko bado zile enzi za kukomeshana zinaendelea katika zama ambazo timu iko katika weledi?

Inawezekana kabisa kusajili mchezaji kwa kutaka kujaza nafasi ili uwe nakikosi kipana cha kushindana na timu kubwa lakini kwa haya tunayo yaona kweli weledi upo.

Morrison hajasajiliwa Simba wala hakuna aliyethibitisha kuwa atasajiliwa ila  ni sehemu muhimu kwa timu kuangalia mchezaji gani anafaa.

Simba inatakiwa  isajili wachezaji  watakao pambana na timu kama Al Ahly, AS Vita na TP Mazembe.

Kwa ligi ya ndani Simba imefanya vizuri na kweli hakuna mpinzani kwakuwa tumeona wachezaji waliowasajili na wanavyotesa ndani ya ligi.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara wanatakiwa wawaze watu kama hao hivi sasa, tayari wameingia katika mikikimikiki ya michuano ya klabu bingwa Afrika ni wakati wa kuchagua wachezaji sahihi.

Nimezungunza na Hassan Mkotya yeye ni mdau wa soka taaluma yake ni Ualimu alitanabaisha kwamba Simba inahitaji  kufanya usajili wa kiweledi sana ili ifike juu.

Kwa sasa inatakiwa isajili wachezaji walio juu ya hawa waliopo ili waweze kupigana na timu kubwa Afrika.

“Simba inatakiwa isajili mchezaji anaye jifahamu sio kama Morrison, wachezaji walio na nidhamu ya hali ya juu ili waweze kufika malengo wanayo yahitaji,” alisema.

Simba itaingia katika michuano ya klabu bingwa Afrika hivi karibuni na kama ilivyo kawaida itapangiwa timu ngumu hapo ndipo katika kipimo cha kuangalia hii timu inayoteaa VPL itatesa tena katika michuano mikubwa..

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
CR

Ronaldo, Messi wanatudai?

Mtibwa

Mtibwa Sugar yaifanya ngazi Azam FC