in , , ,

Inzaghi kocha mpya AC Milan

*Berlusconi amtupia virago Seerdof

AC Milan wamemfukuza kazi Kocha Clarence Seedorf na kumpa kazi hiyo Filippo Inzaghi.
Seedorf amefukuzwa kazi ikiwa ni pungufu ya miezi mitano tu tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo kwa klabu inayocheza Ligi Kuu ya Italia – Serie A.

Mdachi huyu mwenye umri wa miaka 37 alipewa mikoba kwenye klabu aliyochezea kwa miaka 10 tangu 2002.
Inzaghi naye ni mkongwe aliyechezea AC Milan lakini hajapata kufundisha timu iliyo katika ligi kuu. Alikuwa akifundisha timu ya vijana chini ya miaka 19 y AC Milan.

Inzaghi (40) amepewa mkataba wa miaka miwili na ameajiriwa baada ya mmiliki wa klabu na rais wake, Silvio Berlusconi kusema Ijumaa iliyopita kwamba Seerdof ni sehemu ya walioshindwa kazi hapo San Siro. Berlusconi ni waziri mkuu wa zamani wa Italia na ni mfanyabiashara bilionea anayemiliki pia vyombo vya habari.

Enzi za kusakata kwake soka, Inzaghi alichangia kwa kiasi kikubwa Timu ya taifa ya Italia kutwa ubingwa wa dunia 2006, makombe mawili ya Uefa  na makombe matatu kwa AC Milan katika Serie A.

Seedorf alichukua nafasi ya kocha aliyemtangulia, Massimiliano Allegri aliyefukuzwa kazi kutokana na kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu 2013/14. Aliajiriwa akitoka kuchezea klabu ya Botofago ya Brazil, ambapo inaelekea alitundika daluga makusudi kwa kazi hiyo.

Wachambuzi wengi wa masuala ya soka walikuwa na wasiwasi juu ya uteuzi wake na iwapo angedumu kwenye kazi hiyo na kweli amefukuzwa baada ya ligi kumalizika.

Alipoajiriwa AC Milan kama kocha, Seedorf alisema alidhamiria kuirejesha klabu kwenye heshima iliyokuwa nayo awali
AC Milan walmfukuza Allegri baada ya kufungwa na vibonde Sassuolo 4-3 Januari mwaka huu. AC Milan wamekuwa mabingwa wa Italia mara 18 na alipofukuzwa walikuwa nafasi ya 11 na wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya nan echini ya Seedorf.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014

Abramovich kuwatosa Chelsea?