in , , ,

HAPPY ‘Anniversary’ MESUT OZIL

Miaka minne imepita tangia ajiunge na Arsenal kutoka timu ya Real Madrid.

Ulikuwa usajili usiokuwa unategemewa sana kama utafanyika kwa sababu
awali hapakuwa na dalili ya Arsenal kumsajili Mesut Ozil.

Giza la mwisho la tarehe 02/09/2013 ndiyo lilileta mwanga kwenye
kikosi cha Arsenal.

Mwanga ambao mwanzoni ulionekana una wingu la giza kwa sababu
alichelewa sana kuingia kwenye mfumo wa soka la England.

Soka ambalo linahitaji nguvu na kasi kila sekunde ya mchezo. Kucheza
kwake pembeni kushoto kulimfanya achelewe pia kufikia matamanio ya
mashabiki wengi.

Mashabiki wengi walitamani Ozil akitoa pasi nyingi za magoli kama
ilivyozoeleka kwa watu wengi kuwa ni mfalme wa kutoa pasi za mwisho za
magoli.

Unyonge ulitawala ndani ya nafsi yake, akawa hana chochote cha kuwapa
mashabiki zaidi ya kimya chake.

Kimya chake kilikuja na jibu sahihi cha kilio cha mashabiki wengi wa Arsenal.

Arsene Wenger alifanikiwa kumrudisha katika namba yake ambayo Mungu
alimletea duniani.

Namba kumi, namba ambayo ilikuwa na nafasi kubwa kwake yeye kutimiza
matazamio ya mashabiki wengi.

Wengi walitamani kumuona Ozil akitoa pasi nyingi za mwisho pamoja na
kutengeneza nafasi nyingi za magoli.

Miaka minne ya mafanikio kwake akiwa na jumla ya vikombe sita akiwa na
timu ya Arsenal pamoja na pasi za mwisho zaidi ya 40 katika misimu
minne.

Hii ndiyo kazi ambayo Mungu alimleta Ozil kufanya na ndiyo ambayo kila
shabiki wa Arsenal alitamani kumuona Ozil akiifanya.

Ozil amekaa kwenye klabu ambayo wengi wa mashabiki hawataki kumuona
kocha wao Arsene Wenger.

Klabu ambayo mashabiki wake wana kiu ya miaka 13 bila kushinda kombe
la ligi kuu ya England.

Klabu ambayo wachezaji wengi wanashambuliwa na mashabiki, pamoja na
wachezaji wa zamani wa timu hiyo.

Moja ya wachezaji ambao wanashambuliwa kwa kuwa mzembe uwanjani ni Ozil.

Lakini Ozil hajawahi kukatishwa tamaa na maneno haya, amekuwa mtu
ambaye kila siku akipigana ili aitumikie klabu yake ya Arsenal.

Klabu ambayo inaonekana ipo moyoni mwake kwa sababu husimama mbele ya
jamii na kuitetea pamoja na kusema wazi ana furaha kuwepo ndani ya
timu.

Hajawahi kukatishwa tamaa na maneno mabaya , hajawahi kufikiria kuhama
ingawa kuna dalili ya kutoongeza mkataba wake.

Ujumbe wa jana kwa mashabiki wa Arsenal ulionesha ni wa kuwaaga lakini
ametumia busara kubwa sana kuwaaga mashabiki wake.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

IDADI YA WACHEZAJI WALIOSAJILIWA TANGIA DIRISHA LIFUNGULIWE NA KUFUNGWA LEO

Tanzania Sports

NDEMLA FUTA VUMBI KWENYE KIOO