in

Goli La Sabiyanka Halifanani Na Morrison

Sabiyanka


Ikiwa kila mmoja yupo ‘Busy’ kuangalia rekodi mbalimbali za ligi pamoja na magoli huku wengine wakijiwajibisha kutafuta ‘Angle’ ya habari juu ya mikikimiki ya michuano hii.


Tutakuwa wachoyo wa fadhila kumuandika nyota wa Tanzania Prisons kufunga goli la kwanza kabisa la ufunguzi  wa Uwanja wa Mkapa.


Ieleweke hivi, tangu jina la uwanja huo libadilike kutoka uwanja wa Taifa hadi kuitwa uwanja wa Mkapa, katika mechi rasmi ya mashindano mchezaji aliyeufungua kwa kufunga goli ni Lambert Sabiyanka.


Utofauti wa goli la Morrison na Sabiyanka ni kwamba hili la Morrison limefungwa dakika ya 44 likiwa katika mchezo wa kirafiki huku Sabiyanka amefunga dakika ya nane na likiwa la mashindano.


Hivyo basi katika goli la mashindano rasmi tunalihesabu hili la Sabiyanka wa Tanzania Prisons.
Sabiyanka amefunga goli la historia dakika ya 8 wakati timu yake ya Tanzania Prisons ilipokuwa inacheza na Yanga katika uwanja huo.


Na rekodi yake ikawa nzuri zaidi kwani katika raundi ya kwanza ndio lilikuwa goli lililofungwa dakika za mapema zaidi hadi Enock Jiah alipofunga goli la ushindi dakika ya 7 kati ya timu yake ya Ihefu dhidi ya Ruvu Shooting raundi ya pili.


Hivyo ni rahisi kusahau matokeo mengine lakini sio kusahau rekodi hii bora kabisa.
Jamani hebu tumpe heshima yake Sabiyanka tumuandike na tumtambulishe kwa kile kizuri alichokifanya.


Tuliwahi kuandika hapa kuwa goli la kwanza katika uwanja huu ulipofunguliwa mwaka 2007 lilifungwa na Abdi Kassim ‘Babi’ dhidi ya Uganda ulikuwa mchezo wa kirafiki.
Lakini goli la mashindano lilifungwa tena na Abdi Kassim alipokuwa anacheza Azam FC katika michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho.


Hadi sasa uwanja wa Mkapa umeshuhudiwa ya kifungwa magoli 7.
Simba wamefunga magoli 4 wakati huo Yanga wamefunga 2 na Tanzania Prisons wamefunga goli moja.


Magoli ya Simba yamepatikana katika mchezo walioupiga dhidi ya Biashara United.
Lakini uwanja huu tangu ubadilishwe jina uliwahi kutumiwa katika mechezo ya kirafiki na goli la kwanza katika mechi ya kirafiki lilifungwa na timu ya Simba ilipokuwa inacheza na Vital O ya nchini Burundi mfungaji wa goli la kwanza alikuwa ni Benard Morrison kipindi cha kwanza.


Na hapa sasa unapata ule utofauti  wa goli la Morrison na Sabiyanka ni kwamba hili la Morrison limefungwa dakika ya 44 likiwa katika mchezo wa kirafiki huku Sabiyanka amefunga dakika ya nane na likiwa la msahindano  kama tulivyoeleza huko juu.


TAKWIMU SASA


Magoli 14 yamefungwa katika raundi ya 3 kama ilivyokuwa raundi ya kwanza huku ile ya pili yalipatikana mawili.
Katika magoli 14 ya raundi ya pili saba yamefungwa kipindi cha kwanza na saba yamefungwa cha pili.


Simba imechangia magoli mengi katika hatua hii kwani imefunga magoli 4 kama ilivyofanya KMC katika raundi ya kwanza.
Jumla magoli 41 yamefungwa katika raundi zote tatu za ligi kuu Tanzania Bara.
KMC inaongoza kwa kutupia kwani imetupia magoli 8 ikifungwa mawili ikifuatiwa na Simba iliyopata magoli 7 na kufungwa mawili.


Pricne Dube, Kabunda ,Lusajo Reliant Mzamiru Yassin na Chama kila mmoja amefunga magoli mawili.
Lakini Dube, Lusajo na Chama magoli yao ya kipekee kwani wameyafunga katika mechi moja.


Hakuna mchezaji aliyefunga magoli matatu katika mechi moja yaani ‘Hat-trick’.
Shika hii, katika raundi ya kwanza yamefungwa magoli 14 yakiwa 9 yamepachikwa kipindi hcha kwanza na matano (5) kipindi cha pili.


Raundi ya pili yamefungwa magoli 13, ikiwa 9 yamepachikwa kipindi cha pili na manne (4) kipindi cha kwanza.


Raundi ya tatu katika magoli 14, yamegawanyika sawa sawa 7 cha kwanza huku 7 cha pili.
Tuyagawe sasa hayo magoli 41, yaliyofungwa kipindi cha kwanza ni 16 wakati cha pili 25.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga, Simba Na Azam Zaokolewa Na Wageni

Tanzania Sports

Samatta Aandaliwe Kisaikolojia