in

Faida mechi za nyumbani

LIGI Kuu ya England (EPL) inarudi kwa kishindo, ambapo leo pazia linafunguliwa na Aston Villa wanaokipiga dhidi ya Sheffield United kisha Manchester City kuwakaribisha Arsenal pale Etihad.

Mechi hizo zinarejea bila washabiki uwanjani, lakini zote zitarushwa na vituo mbalimbali vya televisheni, baadhi zikiwa ni bure. Villa wanatarajiwa watamtumia mshambuliaji wa kwanza wa Tanzania kukipiga EPL, Mbwana Samatta, akitaka kuuonesha ulimwengu wa soka umahiri wake.

Inasubiriwa kuonekana ikiwa kukosekana washabiki baada ya janga la virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu kupungua kusambaa na watu waliougua Covid-19 kupona, huku wengine kwa maelfu wakipoteza maisha sehemu mbalimbali duniani.

Ni wazi kwamba kuwapo kwa washabiki siku zote kumekuwa na faida kwa timu husika, wakiwatia moyo wachezaji, wakiwashangilia na kuwapandisha morali hata wakashinda mechi. Ukweli wa hiyo umeshaonekana nchini Ujerumani, ambako Ligi Kuu – Bundesliga ilisharejea baada ya nchi hiyo kumudu kwa ustadi virusi vya Corona.

Tanzania Sports
Kocha wa Arsenal akiwa kazini

Si ajabu ikawa tabu kwa timu zinazocheza nyumbani kupata ushindi, wachezaji wakitazama jinsi majukwaa yalivyo tupu. Kabla ya janga la Corona, timu za Ujerumani zilishinda kwa asilimia 43.3 za nyumbani. Baada ya janga hilo, takwimu hiyo imeshuka hadi asilimia 21.7. Hii ni sampuli ndogo sana lakini takwimu kama hizo zimesharekodiwa kwenye ligi nyingine za Ulaya.

Wakati takwimu zinaonesha hivyo, silika inaonesha hivyo pia. Mazingira yasiyo rafiki kwa timu za nyumbani huziathiri kwa kiasi kikubwa, na safari hii inadhaniwa kwamba hakutakuwapo faida kwa timu za nyumbani.

Hata hivyo, wachezaji kwa kawaida huwa wanabeza athari ya washabiki, na wakiwa ni wa kulipwa wanaojali taaluma yao, hawapendi kuzungumza hadharani wakati wakiwa bado wanacheza, lakini baada ya kustaafu hueleza hali halisi ilivyo.

Nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry, amejitokeza na kuandka kwenye tawasifu yake jinsi hali ilivyokuwa, kwenda Anfield kuwakabili Liverpool kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) 2005, akisema hakupata kusikia chochote kama ilivyokuwa Anfield na hatarajii kusikia tena. Yeye na wachezaji wenzake walikuwa katika hali mbaya usiku huo Anfield ikizizima. Chelsea walifungwa 1-0.

Ni kawaida kwa Anfield kulipuka kwa fashifashi usiku kama huo mkubwa, na wachezaji huwa na moyo mkuu, wakicheza kwa ari kuhakikisha kwamba hawawaangushi wachezaji wao. Hisia zinakuwa juu sana nyakati hizo na Chelsea wakashindwa kuhimili hali hiyo. Liverpool hawakuwa wakipewa nafasi kubwa kwenye mechi hiyo, lakini washabiki walibadili hali ya hewa na matokeo kwa ujumla.

Ukosefu wa washabiki viwanjani husababisha timu iliyo nzuri kushinda na hivyo hakuna faida kwa timu ya nyumbani. Hii itawapa wakati mgumu yimu kama Watford kupata alama kutoka kwa City watakapokutana Julai pale Vicarage Road. Ushindi wa Hornets dhidi ya Liverpool uliowashangaza wengi mbele ya washabiki wa hao wa awali, hautarajiwi tena katika viwanja vitupu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Nugaz

Nugaz na Bumbuli hawafanyi kazi ofisi moja?

Moro kaigharimu Yanga

Moro aigharimu Yanga VPL