in

Fahamu mambo muhimu Kombe la Dunia 2022

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ni miongoni mwa mastaa wa  Kiafrika watakaokosa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022. Tanzania ilimaliza katika  nafasi ya tatu kwenye Kundi J ikiwa imejikusanyia pointi 8 nyuma ya Benin na DRC.  

Kinara wa kundi hilo alikuwa DRC wenye pointi 11 akifuatiwa na Benin wenye pointi 10.  Wapo nyota kadhaa kutoka bara la Afrika, Asia,Ulaya na Amerika ambao huenda  wakakosa fainali hizo za kusisimua ambazo hufanyika kila baada ya miaka minne.  

Nazo Italia na Ureno zinahaha kutafuta nafasi ya kucheza fainali hizo mwakani. Makala  haya yameandikwa kabla ya kujua hatima ya Ureno na Italia ikiwa zitashiriki fainali hizo  au la.  

Hivyo kama Italia itashindwa kufuzu ina maana itakuwa mara ya kwanza bingwa wa  Euro kukosa fainali za Kombe la Dunia. Hata hivyo kuna habari nyingi kuelekea fainali  hizo ambazo zinatajwa kuwa za kipekee. 

TANZANIASPORTS inaangazia masuala muhimu kuelekea fainali hizo za kukata na  shoka ambazo zinatajwa kuwa za gharama kubwa za maandalizi kuliko fainali  nyinginezo. Yafuatayo ni mambo muhimu unayopaswa kujua katika fainali hizo. 

Mosi, hizi zitakuwa Fainali za kwanza za Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya  Kiarabu. Fainali hizo tangu zimeanzishwa hazijawahi kufanyika katika nchi ya Kiarabu,  kwahiyo mwenyeji wake Qatar ndiye wa kwanza katika ukanda huo kama ilivyokuwa  kwa bara la Afrika ambapo Afrika kusini ilikuwa ya kwanza kuandaa fainali za Kombe la  Dunia.  

Pili,kwa kawaida Fainali za Kombe la Dunia huwa zinafanyika katika miezi ya Juni na  Julai. Katika fainali za mwaka 2002 nchini Japan na Korea kusini baadhi ya mechi  zilichezwa asubuhi kwa saa za Tanzania.  

Watanzania walikuwa wakiamka na baada ya chai wakajikuta wanatakiwa kutaza mechi  za Fainali za Kombe la Dunia kutokana na tofauti ya muda. Kwa kuzingatia hilo la  muda, sasa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 zitachezwa mwezi Desemba ili  kuepuka hali ya hewa ya joto kali katika miezi ya Juni na Julai nchini Qatar. Itakuwa  mara ya kwanza kwa fainali za Kombe la Dunia kuchezwa mwezi Desemba. 

Tatu, wenyeji Qatar wamepanga kujenga vituo viwili vya umeme wa sola kama sehemu  ya kuongeza nguvu za umeme mwingine katika vituo mbalimbali nchini humo. 

Nne, sheria za Qatar zinapiga marafuku watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja  hivyo uwezekano wa wao kuhudhuria fainali hizo ni mdogo mno. Lakini mamlaka za 

serikali ya nchi hiyo zimesema hakuna mashabiki watakaozuiwa kuingia nchini humo  kushuhudia fainali hizo.  

Nne, uuzaji wa pombe utakuwa katika maeneo maalumu wakati wote wa fainali za  Kombe la Dunia mwaka 2022. Hivyo hazitapatikana kila mtaa. 

Tano, hizi Fainali za pili za Kombe la Dunia kufanyika katika bara la Asia. Mwaka 2002  fainali hizo ziliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Japan na Korea kusini ikiwa ni mara ya  kwanza. 

Sita, kabla ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022, nchi mwenyeji Qatar imeandaa  mashindano maalumu kwa mataifa ya Kiarabu ambayo yanatarajiwa kufanyika jumanne  ya Novemba 30 mwaka huu. Mashindano hayo yanaitwa FIFA Arab Cup Qatar 2021,  ambapo jumla ya mataifa 16 ya Kiarabu yatashiriki na kuchezwa katika uwnaja wa Rasu  Abu Aboud 974. 

Saba, staa wa zamani wa Cameroon na Barcelona, Samuel Eto’o na Cafu wa Brazil ni  mabalozi wa Qatar katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022. Nyota hao  wametabiri kuwa mwenyeji wa fainali hizo atafika nusu fainali. 

Nane, Qatar inakuwa nchi ya kwanza kutoka mashariki ya Kati kuandaa fainali za  Kombe la Dunia. Pia ni fainali za kwanza kuandaliwa na nchi ya kiarabu na yenye  utamaduni wa kiiaslamu. 

Tisa, fainali hizo zitachezwa katika viwanja vya Al Thumama,Lusail,Al Janoub,Qatar  Foundation Stadium,Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa,Al Bayt,Ahmad Bin Ali na Ras  Abu Aboud. Jumla ya viwanja nane vitatumika katika fainali hizo. 

Kumi, licha ya ksuhutumiwa kuvunja haki za binadamu, Shirikisho la Soka Duniani  FIFA lilikataa kuyumbishwa na kelele za wanaharakati kwa kusimama kidete kuwa  Qatar ndiyo nchi mwenyeji wa fainali za mwaka 2022.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Makocha wanaowindwa Manchester United 

Tanzania Sports

Ukubwa wa sifa za makocha ni ubora wa Ligi Kuu Bara