in , , ,

Fabregas aonekana London


*Yabainika anajiandaa kwa usajili EPL
*Loic Remy aelekea kujiunga Arsenal

Siku moja baada ya taarifa kwamba Barcelona wanamuuza Cesc Fabregas kwa pauni milioni 30, Mhispania huyo ameonekana jijini London.

Fabregas (27) alikuwa nahodha na kiungo mahiri Arsenal kabla ya kurudi nyumbani kwao Hispania na sasa kuonekana London kumezua hisia kwamba atajisajili na moja ya miamba ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Inatambulika kwamba Manchester United walikuwa wakimtaka tangu msimu uliopita, sasa Manchester City wameeleza kumtaka pia huku Arsenal nao wakidhaniwa watamchukua, maana kifungu cha mkataba wake kinawapa wao kipaumbele.

Tayari amewaambia wakuu wake wa Camp Nou kwamba anataka kuondoka sawa na matakwa yao ya kumuuza ili wanunue mchezaji mwingine. Yumo pia kwenye kikosi cha timu ya taifa cha Kocha
Vicente Del Bosque.

Kombe la Dunia limebakisha siku 11 tu kuanza hivyo hawezi kuwa London kwa mapumziko bali kwa shughuli muhimu ya usajili Arsenal au kukutana na maofisa wa klabu nyingine.

Kocha mpya wa Barcelona, Luis Enrique aliweka wazi tangu alipoanza kazi kwamba Fabregas hayupo kwenye mipango yake ya msimu ujao.

Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward amekuwa katika jitihada za kunasa saini yake tangu mwaka jana. Aliporudi Barcelona 2011 akitoka Arsenal, Fabregas alisema ilikuwa changamoto kubwa zaidi katika maisha yake, na kweli miaka miwili tu baadaye anauzwa. Alifunga mabao tisa katika mechi 48 msimu uliopita ambapo Barca hawakutwaa taji lolote.

LOIC REMY AELEKEA EMIRATES

Katika tukio jingine, Arsenal wanadaiwa kumalizana na mshambuliaji wa Queen Park Rangers (QPR) ili ajiunge nao msimu ujao.

Remy amekuwa London kwa muda na pia alikuwa uwanjani Emirates katika mechi baina ya Arsenal na West Bromwich Albion mwishoni mwishoni mwa msimu wa ligi, akakaa upande wa Arsenal.

Remy (27) alikuwa akiwindwa na Liverpool na Tottenham Hotspur lakini yaelekea Arsenal wamewazidi kete kwa kumalizana na Mfaransa huyo aliyechezea Newcastle kwa mkopo msimu uliopita.

Inadaiwa kwamba kama mambo yatakwenda sawa, Kocha Arsene Wenger atawalipa QPR ada ya kwenye pauni milioni 10 ili kumchukua Remy.

Alikuwa mfungaji bora Newcastle msimu uliopita, ambapo alitikisa nyavu mara 14 katika mechi 26 na muda mwingine alikuwa majeruhi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wachezaji lazima waimbe Wimbo wa Taifa

Hayatou angโ€™aka mlungula wa Fifa