in , , ,

Eto’o awaunganisha Cameroon

NYOTA wa Chelsea, Samuel Eto’o amewataka wadau wote wa soka wa Cameroon kuungana ili nchi yao ifuzu kwa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Mwito wa Eto’o unakuja katika hali ya kushangaza, kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa haelewani na kocha kiasi cha kujitoa kwenye timu ya taifa kabla ya kurejea.

Indomitable Lions wanaoyumba siku hizi wanahitaji ushindi wa aina yoyote, maana katika mechi ya kwanza ya mtoano dhidi ya Tunisia walikwenda suluhu na Jumapili hii wanarudiana ambapo Eto’o ameapa kuweka kando tofauti zake za siku nyingi na Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) ili kujituma kuivusha nchi yake.

Eto’o anadai kwamba wachezaji wenzake walimbagua na kukwepa kumpasia mpira katika mechi ya awali na anasema kuna mkanda wa video kuthibitisha hilo.

“Hebu tuzike tofauti zetu ili timu yetu ifuzu kwenda Kombe la Dunia … ni kufa au kupona Jumapili, lazima tuwe wamoja, si lazima mimi nifunge mabao japokuwa nimeifanya kama tabia yangu, sina ubinafsi hata kidogo,” akasema nahodha huyo wa Indomitable Lions.

Hata hivyo, Kocha Mjerumani, Volker Finke alionekana kutomaizi kutokea vitendo hivyo uwanjani lakini anaiweka timu pamoja kwa ajili ya kufanya vizuri Jumapili.

Eto’o anasema soka ni jambo kubwa na muhimu kwa Cameroon na nchi kwa ujumla, hivyo wakiondoa tofauti zao itakuwa vyema wakishinda potelea mbali hata kama wengine hawatamsalimu baada ya mechi hiyo.

“Wale wanaolitetea Shirikisho na wale wanaolipinga tuelewe kwamba sote ni Wacameroon na sitaki kuona habari za ajabu kutushambulia kabla ya mechi hii. Lazima tufanye kila kitu Jumapili ili kufuzu,” akasema Eto’o.

siku zilizopita pamekuwapo mikwaruzo kati ya
Eto’o na wachezaji wenzake na pia dhidi ya Fecafoot, ambapo Eto’o amekuwa akipinga jinsi timu hiyo ya taifa inavyoandaliwa na kuedneshwa.

Eto’o (32) alitumikia adhabu ya kutochezea timu ya taifa kwa muda baada ya kubainika kushawishi wenzake kugoma na pia kiburi chake dhidi ya Fecafoot.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Shabiki Arsenal apoteza nyumba

Penati ya Chelsea yawasha moto