in

England kwaheri….

Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.

Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.

Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.

Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda Italia.

Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.

Kadri mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio za kutegemewa tena.

Baada ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: “Wachezaji walicheza kadri ya uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti, lakini mambo hayakuwa hivyo. Ukiongoza katika penalti, unashikilia matumaini kwamba mambo yatasalia hivyo, lakini Italia ndio waliokuwa na bahati. Vijana waliokuwa walinzi walifanya kazi nzuri mno, na kuiletea nchi fahari, lakini tunarudi nyumbani na mioyo ya huzuni, na hili ni jambo gumu kulikubali.”

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Taifa Stars back on track

Jacob Mulee ataka athaminiwe kama makocha wazungu…….