in

El Clasico mikononi mwa Munuera

Martinez Munuera

El Clasico mikononi mwa Munuera 

nani kucheka au kununa? 

Jumamosi ya wiki hii dunia nzima itaelekeza macho na masikio katika uwanja wa  Camp Nou jijini Barcelona kati ya miamba miwili ya soka nchini Hispania.  Barcelona watakuwa na staa wao Lionel Messi akiwa anaingia msimu wa tatu bila  mshindani wake wa karibu Cristiano Ronaldo. 

Huo utakuwa mchezo wa 7 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Hispania msimu huu  2020/2021. Huku timu zote zikiwa na mwelekeo wa kutaka kuibuka washindi wa  Ligi hiyo mwishoni. 

Real Madrid itaingia uwanjani ikiwa imejeruhiwa mara mbili; kwanza ilifungwa  kwenye mchezo wa mwisho wa La Liga dhidi ya Cadiz. Pili imezabwa mabaom3-2  dhidi ya Shakhtah Donesk kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa  Ulaya. Barxcelona wataingia uwanjani wakiwa na kocha mpya Ronald Koeman,  huku Madrid wakiendelea kutegemea ‘uchawi’ wa Zinedine Zidane, ambaye pia ni  bingwa mtetezi wa Ligi hiyo. 

EL CLASICO BILA SHANGWE 

Mchezo huu ni kama ‘derby’ ya Ligi yoyote ile. Ni kama Olrando Pirates na  Mamelodi Sundowns au Kaizer Chiefs. Ni kama Yanga na Simba, AC Milan na  Inter Milan. Ni pambano la wapinzani wa jadi ambao wanataka kutangaza zaidi  ufalme wao. 

Katika pambano hili mashabiki wakiwa wameketi kwenye viti au masofa yao yao  nyumbani watashuhudia pambano la kwanza la wapinzani wa jadi bila kujazana  uwanjani. Pambano hili linakwenda kuweka historia kuwa El Clasico ambayo  mashabiki hawakuruhusiwa kuingia uwanjani.  

Sababu inakuwa ni moja tu; kuepuka kuambukizana zaidi ugonjwa corona. Si  mashabiki wa wenyeji wa Barcelona wala wageni Real Madrid. Hakuna mauzo ya  tiketi kwa vle hawaruhusiwi kuingia uwnajani. Hakuna mauzo ya vinywaji  uwanjani. Hakuna amsha amsha uwanjani. Hakuna zomea zomea uwanjani. Vtote  hivi vinakosekana sabababu ya corona. 

Katika pambano hilo kila upande utakuwa na hamu ya kushinda. Ronald Koeman  atataka kuwadhihirishia mabosi wake wa Barcelona yu kocha sahihi kuokoa jahazi  la klabu hiyo ambalo linadidimia siku hadi siku.  

Kwa upande wake Zinedine Zidane atataka kuweka rekodi ya kutofungwa kwenye  uwanja wa Camp Nou. Zidane hajawahi kufungwa ndani ya dimba hilo tangu awe  kocha wa Real Madrid kwa awamu zote mbili. Je makocha hao watamudu  kutambiana? Majibu yatapatikana baada ya mchezo. 

FILIMBI YA MUNUERA 

Kwenye mchezo wa El Clasico, mtu mmoja atakuwa ameshika filimbi katikati ya  dimba akichezesha mechi hiyo kwa dakika zote 90. Mtu huyo ni Martinez  Munuera. Chama cha soka cha Hispania, RFEF kimetanagza kuwa Munuera ndiye  atachezesha mechi ya El Clasico. 

Wakati Munuera akishika filimbi kwenye pambano hilo, ndani ya chumba cha  VAR atakuwapo mwamuzi mwingine Martinez  Munuera

Munuera amechezesha mechi 24 za Real Madrid tangu alipoanza kazi ya uamuzi  La Liga. Kati ya mechi hizo imeshinda mechi 15, kutoka sare mechi 8 na  imeambulia vipigo katika mechi 4. Mchezo wake wa mwisho kwa Real Madrid  ulikuwa walipopambana na Real Sociedad msimu huu. 

Aidha, Munuera amechezesha mechi 21 za Barcelona dhidi ya timu mbalimbali.  kati ya mechi hizo Barcelona imeshinda mara 15 sawa na Real Madrid. Barcelona wenyewe wametoka sare mechi 3 na kuambulia vipigo katika mechi 3. Mchezo  wake wa mwisho kuwaamua Barcelona ulikuwa msimu uliopita walipocheza dhidi  ya Leganes na kushinda mabao 2-0. 

Katika mechi za Real Madrid amewapa kadi za njano wachezaji watano, wakati  Jesus Vallejo peke yake alilimwa kadi nyekundu. Hivyo ni refa ambayo ni mkali  kwa wachezaji na inawalazimu kuwa waangalifu mara mbili ya hali ya kawaida. 

Munuera kwa sasa ana umri wa miaka 38. Amechagyliwa kuchezesha mechi ya El  Clasico kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu huu. Uchezeshaji ambao  uko mbali na malalamiko, usahihi wa kutafsiri sheria na kuwa karibu kila mahali  ambako makosa hufanywa na wachezaji.

Kwa maana hiyo msimu huu Munuera anaweka rekodi ya kuwa mwamuzi wa  kwanza kuchezesha El Clasico ikiwa tupu. Ni El Clasico isiyo na mashabiki  uwanjani. Huenda hii itakuwa histoia yake ya kusimulia wajukuu miaka ijayo.  

Na zaidi ni ndiye mwamuzi atakayetajwa miaka ijayo kuwa alichezesha mechi  isiyo na mashabiki kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa corona. Ni corona  itamweka kwenye ramani, lakini uamuzi bora ndiyo utakuwa na thamani kubwa.  

Kwenye pambano hili timu zote zinaingia zikiwa na mapungufu kadhaa. Zote  zimekuwa na viwango dumu katika mechi za karibuni. Zote zinajaribu kujijenga  zaidi. Barca wamemuuza mshambuliaji wao Luis Suarez, wakati Real Madrid  haijasajili mchezaji yeyote.  

Hii ni mechi ya kuoneshana umwamba na kutafuta ufalme. Ni nani ataibuka  mshindi kati ya kocha mpya wa Barcelona au Zidane kuendeleza rekodi yake ya  kutofungwa Camp Nou? Majibu yatakuja baada ya mechi.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Benjamin Mkapa Stadium Dar

Yanga hakuna, Simba hakuna

Tanzania Sports

Azam Bingwa Chini Ya Yanga Na Simba