in , , ,

Drogba wingu jeusi Ulaya

*Kibali chake Ligi ya Mabingwa shakani

 

Didier Drogba ameingia matatani, kwa madai ya kuchezea Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) bila ruhusa.

Klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani iliyotoka sare ya bao 1-1 na Galatasaray Jumatano hii, imefungua rasmi malalamiko yake dhidi ya mchezaji huyo wa Ivory Coast.

Drogba alijiunga Galatasaray akitokea Shanghai Shenhua alikocheza kwa muda mfupi na kutokea utata wa mkataba na malipo yake.

Shenhua pia ililalamika FIFA kwa maelezo kwamba Drogba ameondoka kinyume na mkataba unaomfunga nao bado, lakini FIFA ilitupilia mbali na kumwidhibisha kuchezea Galatasaray ya Uturuki.

Katika mechi hiyo ya Ligi ya UCL ambayo Galatasaray walikuwa wenyeji, Drogba alicheza kwa dakika 90.

“Kuna shaka juu ya uhalali wa kibali cha kumchezesha Drogba kwneye Ligi ya Mabingwa, Schalke 04 wana haki katika hili na wanalishughulikia,” klabu hiyo ya Ujerumani imenukuliwa ikisema.

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limekiri kupokea malalamiko kutoka Schalke 04 juu ya uhalali wa mchezaji huyo kukipiga kwenye ligi yao.

Shirikisho hilo linasema kwamba kamati yake ya nidhamu itakaa na kuchunguza suala hilo, lakini bado tarehe ya kikao haijapangwa.

Drogba alijiunga Galatasaray kwenye dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu, baada ya kukataliwa kuhama kabla ya hapo, alipoona mambo hayaendi sawa China, alikokuwa amejiunga na mwenzake, Nicolas Anelka ambaye pia ameondoka.

Drobga amesaini mkataba wa miezi 18 na Galatasaray, wakati Shenhua alikuwa amesaini makubaliano ya kucheza kwa miaka miwili unusu, na alitia saini Juni mwaka jana.

Ameshacheza mechi mbili Uturuki, moja ikiwa ni ya ligi Ijumaa iliyopita, alipoingia uwanjani akitokea benchi na kufunga bao dakika chache tu baada ya kuingia.

Drogba aliondoka Chelsea kwa sherehe ya kutwaa ubingwa wa Ulaya na klabu hiyo ya Uingereza, ambapo mkwaju wake wa penati uliokuwa wa mwisho, ndio uliowapa rasmi Chelsea taji.

Majuzi ametoka nchini Afrika Kusini, alikokuwa na timu ya taifa ya Ivory Coast – Tembo, lakini hawakufanya vizuri walivyotarajiwa, kwani waliishia robo fainali, walikotolewa na mabingwa wapya, Nigeria.

 

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barcelona mbendembende San Siro

Atletico watema ubingwa Europa