in , , ,

Dondoo za kombe la Dunia….

Kombe la dunia ni tukio ambalo huleta hisia za watu wengi kuwa pamoja,
watu hukutana kwa pamoja na kuzungumza lugha moja ambayo huwa inakuwa
yenye hisia moja ambayo ni mpira.

Tangu mwaka 1930 lilipoanza kombe hili la dunia nchini Uruguay, watu
wengi wamekuwa wakitamani kuweka historia ya pamoja.

Kumbukumbu nyingi hubaki vichwani mwao kila kombe la dunia linapoisha,
kumbukumbu ambazo hubaki kama simulizi kwa vizazi mbalimbali.

Kumbukumbu ambazo zina matukio ya kila aina mazuri au mabaya
yanayotokea nje na ndani ya uwanja.

Baadhi ya nyota wa soka, wa mataifa yatakayo shiriki kombe la Dunia Urusi.

Kuna matukio mengi sana ambayo sisi huyakumbuka kirahisi yanapotokea
ndani ya uwanja kwa sababu wengi huyaona na wengi macho yetu
huyaelekeza huko kwa sababu shauku yetu huwa kutazama burudani
inayotokea ndani ya uwanja.

Ila kuna vitu vingi nyuma ya pazia hutokea kwenye kombe la dunia, ni
ngumu kwa mtu kuviona au kuvisikia kwa wingi kwa sababu vinatokea
nyuma ya pazia.

Wengi macho yetu huishia kwenye matukio yanatokea ndani ya uwanja, na
kumbukumbu zetu hujazwa matukio ya magoli, timu kushinda au kushindwa
lakini kuna matukio yanayotokea nje ya uwanja ambayo wengi watu wengi
hawayajui.

Yafuatayo ni matukio saba (7) ambayo yamewahi kutokea nje ya uwanja na
wengi wetu hatuyajui.

1: Mchezaji haruhusiwi kufanya tendo la ndoa kipindi cha kombe la
dunia, inasemekana mchezaji humaliza nguvu nyingi anapofanya tendo la
ndoa hivo makocha wengi huwa wanawafungia wachezaji wanaofanya tendo
la ndoa kipindi cha kombe la dunia, na ikizingatia mashindano ya kombe
la dunia hutumia muda mfupi na ratiba za mechi huwa karibu karibu hivo
makocha wengi huwa wanatoa onyo kwa mchezaji anayefanya ngono kipindi
hiki kwa kuhofia kupoteza nguvu nyingi kipindi hiki.

2: Dunia inakadiliwa kuwa na watu bilioni 7.5, watu bilioni 3.2
huangalia kombe la dunia ambapo ni sawa na asilimia 46% ya watu wote
duniani ambapo inakaribia kuwa 50% ya watu wote duniani.

3: Kwenye kombe la dunia kuna aina Milioni 3 za bia zinazouzwa, kwenye
kombe la dunia la mwaka 2010 lita 750,000 za bia ziliuzwa , wengi
wa mashabiki hujenga urafiki na undugu ambao husababisha kupata muda
wa pamoja kunywa vinywaji mbali mbali kama bia ambapo ndicho kinywaji
ambacho hutumiwa kwa kiasi kikubwa na mashabiki wanohudhulia kombe la
dunia.

4: Kombe la dunia husababisha ongezeko la kuzaliana kwenye nchi
inayoandaa kombe la dunia, mfano miezi tisa baada ya kombe la dunia la
mwaka 2006 nchini Ujerumani, watu walizaa kwa ongezeko la asilimia 10,
na hii ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kwenye kombe la dunia na
miingiliano ya watu wa mataifa mbalimbali ambao husababisha kushamiri
kwa tamaa za ngono.

5:Kila timu inayoishia hatua ya makundi hulipwa dollar milioni 8,
mshindi wa kombe la dunia hulipwa dollar Milioni 35 na mshindi wa pili hulipwa
dollar milioni 25, kwa kifupi hakuna timu inayotoka kapa kwenye kombe
la dunia.

6: Viwanja vingi vinavyojengwa kwa ajili ya kombe la dunia hujengwa
nje ya mji, mfano viwanja 12 vilivyotumika kwa ajili ya kombe la dunia
la mwaka 2014 vilikuwa na umbali wa 1,997 miles kutoka makao makuu ya
miji iliyotumika kama mwenyeji wa kombe la dunia.

7: Kombe la dunia la mwaka 2014 ndiyo lilitumia gharama kubwa sana
kwenye maandalizi, ambapo lilitumia dollar za kimarekani bilioni 14.5.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KUKOSEKANA KWA NEYMAR KWENYE MICHEZO YA KIRAFIKI NI FAIDA KWA BRAZIL

Tanzania Sports

RAPHAEL DAUD, NI NGUMU KUONA MAWIO KWENYE TAA ZA KARIAKOO