Dnipro, Sevilla fainali Europa

Fainali ya Ligi ya Europa itawakutanisha Dnipro na mabingwa watetezi, Sevilla baada ya Dnipro kuwachapa Napoli.

Mshambuliaji wa Ukraine, Yevhen Seleznyov ndiye alifunga bao pekee katika mchezo huo. Fainali itachezwa jijini Warsaw, Poland Mei 27.

Sevilla walio Ligi Kuu ya Hispania walikamilisha kazi yao kwa kuwachapa Fiorentina 2-0 na kuwatoa kwa uwiano wa mabao 5-0.

Kuingia nusu fainali kwa Fiorentina na Napoli kulitoa uwezekano wa timu za Italia kucheza fainali hivyo kujihakikishia kutwaa kombe, lakini walipoteza fursa hizo.

Katika kipindi cha miaka 10 Sevilla wametwaa ubingwa huo mara tatu na sasa wanasaka kuweka rekodi ya kipekee Ulaya kwa kulitwaa mara nne.

Mshindi atafuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

UCL ndiyo michuano mikubwa zaidi Ulaya, yenye heshima kubwa na fedha, ambapo timu za ligi mbalimbali hupambana kufuzu.

Comments