in , ,

SPECIAL OLYMPICS TANZANIA.

Ni miongoni mwa vyama vichache nchini vinavyopata ruzuku ili kuendeleza michezo ya walemavu wa akili.

Special Olympics Tanzania kilianza rasmi mwaka 1968 na aliyekuwa mkurugenzi Ustawi Jamii Ndugu Madai Nyapule mara tu baada ya kurudi masomoni Marekani.

Chama hicho kilianzishwa kwa msukumo mkuu toka kwa Sargent Major Shriver na mkewe Mama Shriver  kwenda kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mwalimu Julius Nyerere.

Sargent Shriver alikuwa mwanzilishi wa shirikisho hilo toka Marekani. Mkewe Shriver ni dada wa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani John F Kennedy. Bila shaka wengi wanakumbuka uhusiano wa karibu kati  ya Mwalimu Nyerere na familia ya John F Kennedy.

Kwa pamoja waliazimia kuanzishwa  kwa chama hicho nchini ili kitoe fursa kwa watu wenye ulemavu wa akili.

Mzee Shriver ambaye pia ni mkwe wa mcheza sinema maarufu marekani  Shwarznigger alifariki mapema mwaka jana .Hata hivyo ndoa ya Shwarsnigger na binti huyo wa Shriver nayo haikudumu baada ya kuachana mwishoni mwa mwaka jana kwa kashfa ya Shwarsnigger  kuzaa na mtumishi wa ndani .

Hata hivyo mtalaka huyo na kaka yake ni watendaji wakuu wazuri wa chama hicho kimataifa.

Pamoja na kupata ruzuku yakutosha kupitia  Chama cha Special Olympics Ireland  bado chama hicho kinasusua katika programs zake nyingi katika kushirikisha wanamichezo wake.

Chama hicho kina bodi maalumu ilioteuliwa na mkurugenzi mtendaji Ndugu Frank Macha.

Ukweli bodi hiyo haina maamuzi yoyote mbele ya mkurugenzi mtendaji

Ndugu Macha aliwahi kuwa maneja wa uwanja wa taifa Dar Es Salaam.

Hapo awali aliazimwa na Special Olympics Tanzania lakini kwa vile amestaafu kazi serikalini hivi sasa ni mtendaji wa kudumu katika chama hicho cha walemavu SOT.

Pamoja na kupata ruzuku tosha bado chama hicho hakina mipango madhubuti kuendeleza  michezo kwa walemavu wa akili nchini.

Chama hicho hutumia pesa nyingi kwa posho za safari na mishahara minono badala ya kutumia kuendeleza walemavu wa akili.

Hadi sasa program nyingi za mikoa hazifanyi kazi zake kutokana na ushirikiano duni wa mtendaji mkuu  wa chama hicho.

Wataalamu wengi waliofundishwa kukiendesha chama hicho  wengi wamejiengua  au kufukuzwa na mtendaji huyo mkuu. Bahati mbaya zaidi chama hicho hakina mkutano mkuu wa wanachama wala uchaguzi wa viongozi  wake  hivyo kutobadili uongozi na haswa wa juu hadi hapo watakapo tangulia mbele ya haki.

Ni muda mrefu sasa chama hicho hakijaendesha mashindano ya taifa  wala kuendesha program zingine kitaifa

Uhusiano wake na vyama vya mikoa  ni mbaya kiasi kwamba linahitajika Baraza la Michezo nchini  kuangalia  upya mienendo ya chama hicho katika kushughulikia walemavu wa akili nchini.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TFF summons clubs to resolve disputed players

Picha za zamani