in , ,

Man United wawalipua Liverpool

Moto wa Manchester United umeendelea kuwaka, ambapo wamewalipua wapinzani wao wa jadi, Liverpool kwa mabao 3-0.

United waliingia uwanjani wakiwa na jeuri ya rekodi nzuri kwenye mechi zilizopita kwa kupata ushindi, hata kama mwingine ulikuwa wa mbinde, huku Liverpool wakiwa hawajiamini kutokana na hali yao mbaya tangu waanze msimu huu.

Vijana wa Louis van Gaal walicheza vyema na kutengeneza nafasi nyingi, ambapo mabao yao yalifungwa na Wayne Rooney, Juan Mata na Robin van Persie anayeelekea kumaliza ukame wake wa mabao kwa kufunga katika mechi ya pili mfululizo.

Wakicheza nyumbani mbele ya maelfu ya washabiki wao, United wameanza kuweka imani kwamba watarejea kwenye soka ya kimataifa msimu ujao kwa kumaliza katika nafasi nne za juu, huku wengine wakiwaza kwamba kuna uwezekano hata wa kutwaa kombe.

Kwa upande wa pili, Liverpool ambao ndio watani wa jadi wa asili kwa miaka mingi wa Man United, wamebaki katika sintofahamu licha ya kutumia mamilioni ya pauni kusajili wachezaji wengi, zikiwa ni jitihada za kuziba pengo la mshambuliaji na mfungaji bora wa msimu uliopita England, Luis Suarez aliyeuzwa Barcelona.

Mario Balotelli, aliyenunuliwa kutoka Milan kwa pauni milioni 16 kama mshambuliaji wa kati, aliingia dakika ya 45 kuchukua nafasi ya Adam Lalana lakini hakuweza kubadilisha mwelekeo wa mechi, sana sana aliambulia kadi ya njano, akiwa ametoka kwenye mapumziko ya majeruhi na kukosa mechi sita.

Katika mechi nyingine, Tottenham Hotspur waliwafunga Swansea 2-1 katika mechi ngumu. Mabao ya Spurs yalifungwa na Harry Kane na Christian Eriksne wakati la Swansea lililokuwa la kusawazisha lilitiwa kimiani na Wilfried Bonny.

Kwa matokeo hayo, Chelsea wanabaki kileleni kwa pointi zao 39 wakifuatiwa na Manchester City wenye 36, Man United 31, West Ham 28, Southampton 26 sawa na Arsenal. Nafasi ya saba ni Spurs waliofikisha pointi 24 wakifuatiwa na Newcastle, Swansea, Liverpool, Stoke na Aston Villa.

Everton wanashika nafasi ya 13 kwa pointi zao 18, wakifuatiwa na sunderland, Crystal Palace, Burnley, Queen Park Rangers, Hull na mkiani ni Leicester.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal, Chelsea, City safi

DROO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA: