in , , ,

Delph atua Man City

*Madrid, Man U wanaendelea kutegeana
*Chelsea wakataliwa ofa ya John Stones

Hatimaye Manchester City wamefanikiwa kumnasa nahodha wa Aston Villa, Fabian Delph baada ya mchezaji huyo kubadili mawazo ya kubaki Villa Park.

Kiungo huyo wa kimataifa wa England amesaini mkataba wa miaka mitano wiki moja tu baada ya kukanusha madai kwamba alikuwa na nia ya kuondoka kwenye klabu yake.

City wamelipa pauni milioni nane zilizokuwa kama sharti kwenye mkataba wake na Villa uliosainiwa Januari mwaka huu.

“Kwa umri wake wa maka 25 tu bado ana muda mrefu wa kuonesha soka safi. Ni mchezaji mahiri na sasa nasubiri kwa hamu kufanya naye kazi,” anasema kocha Manuel Pellegrini.

Baada ya kukamilisha vipimo vya afya Ijumaa hii, anatarajiwa kwenda Australia kuungana na wachezaji wenzake katika ziara kabla ya kuanza msimu ujao.

Washabiki wa Villa wenye hasira waliandamana wakiwa na bango dhidi ya mchezaji huyo nje ya Villa Park, wakimwona kama msaliti aliyeamua kuwatosa dakika za mwisho.

City walikuwa na kiu ya kusajili mchezaji Mwingereza ili kufikia idadi ya wachezaji wa ndani wanaotakiwa kwa klabu za ligi kuu ya England, hasa baada ya kuwaachia Frank Lampard na Micah Richards.

Manchester United na Real Madrid wameendelea kutegeana, kila mmoja akikataa kumtoa mchezaji wake kwa mwingine.

Wakati Madrid wanamtaka golikipa David De Gea, United wamesema hawatamruhusu kuondoka Old Trafford iwapo Madrid hawatawapa beki wao wa kati, Sergio Ramos.

Kwingineko Chelsea wamekataliwa ofa yao ya pauni milioni 20 kwa Everton kwa ajili ya kumpata mlinzi John Stones, 21.

Everton wamewaambia Chelsea ni bora wakaachana na ndoto za kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Barnsley kwa sababu hawana nia ya kumuuza.

Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur na QPR, Harry Redknapp naye amejitokeza akisema kwamba ni bora mchezaji huyo abaki Everton kwa sababu bado anaendelea kujifunza.

Manchester United wanapanga kutoa ofa ya pauni milioni 22 kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Pedro, 27, ambaye pia anatakiwa na Chelsea.

Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema kocha wao, Arsene Wenger, 65, anaweza kubaki klabuni hapo kwa miaka mingine mingi ijayo.

Sunderland wamekamilisha usajili wa Jeremain Lens, 27, na Younes Kaboul, 29, na sasa wanaendelea na malengo yao mengine kujiimarisha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

SCHWENSTEIGER NA SCHNEIDERLIN SI SULUHISHO KAMILI

UZEMBE UNAPOMSHIKISHA SINGANO MAMILIONI YA LEWANDOWSKI