in

David Rudisha, arudi Kenya na Dhahabu, aweka rekodi mpya!

DAVID Rudisha wa Kenya amevunja rekodi ya dunia na kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800.
Rudisha alikimbia kwa dakika moja sekunde 40 na nukta 91 (1:40.01, akivunja rekodi yake aliyoweka 2010 kwa kukimbia 1:41.00.
Rudisha mwenye umri wa miaka 23 anafuata nyayo za baba yake aliyeshiriki katika timu iliyoshirikisha watu wanne kwenye mbio za mita 400 nchini Mexico mwaka 1968 na kutwaa medali ya fedha.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Nijel Amos (18) wa Botswana aliyetwaa fedha, huku Mkenya mwingine, Timothy Kitum akitwaa medali ya shaba.
Rudisha anakuwa mwanariadha wa kwanza kuweka rekodi mpya ya dunia katika Michezo ya London Olimpiki 2012.
Mwanariadha mstaafu wa Uingereza, Denise Lewis aliyepata kutwaa medali ya dhahabu enzi zake, amekaririwa akieleza kustaajabu jinsi Rudisha alivyokimbia.
“Lilikuwa jambo la kuvutia kushuhudia mbio za David Rudisha. Kukimbia kama alivyofanya hapa na katika muda huo kunasisimua, ni maajabu. “Anachotakiwa kufanya sasa ni kwenda na kuchochea kizazi chote cha akina Rudisha wadogo wanaotaka kupata fursa ya kung’aa kwenye jukwaa la kimataifa, ni ajabu sana,” akasema Lewis kwa furaha.
Rudisha ambaye pia ni bingwa wa dunia, aliongoza tangu mwanzo kwenye mbio zilizofanyika usiku wa leo, akiwaacha wenzake umbali wa sekunde 49.28.
Kana kwamba hiyo haitoshi, aliongeza nguvu na kasi hadi akafanikiwa kuivunja rekodi yake mwenyewe na kuweka kiwango kipya cha kimataifa.
Huku washindani wenzake wakijaribu kumfuata kwa kasi kadiri walivyoweza, kila mmoja alifanikiwa kuboresha rekodi zao, isipokuwa Abukaker Kaki aliyeshika nafasi ya saba.
Rudisha alikuwa na haya ya kusema baada ya kushinda:
“Ha! Nimefurahi. Huu ni wakati niliokuwa nausubiri kwa muda mrefu. Kuja hapa na kuvunja rekodi ya dunia ni jambo la ajabu.
“Nilijiandaa vizuri wala sikuwa na wasiwasi juu ya kushinda. Hali ya hewa leo ilikuwa nzuri hivyo nami nikaenda vyema.
“Lord Coe ni rafiki yangu mkubwa na mapema Februari alinizungusha hapa uwanjani. Hilo lilikuwa jambo zuri kwangu, nikadhamiria nije hapa na kufanya kitu ambacho angejivunia,” alisema Rudisha.
Mara baada ya kumaliza mbio hizo za mita 800, Rudisha alinyanyua mikono yake juu kushangilia, huku ubao ukionesha muda aliotumia, na kwamba ni rekodi mpya ya dunia.
Ushindi wake ulipokewa kwa vigelegele na washabiki waliokuwa kwenye Uwanja wa Olimpiki wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000, walifurahia kushuhudia rekodi mpya ya dunia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

David Rudisha atwaa dhahabu

Athletics Tanzania (AT) has embarked on promotion of the athletics through a close partnership with UMISETA.