in , , ,

Conte aelekea Chelsea

Kocha wa Timu ya Taifa ya Italia, Antonio Conte ametua London,
ikielezwa ni kwa ajili ya majadiliano na hatimaye kutia saini mkataba
wa kuwafundisha Chelsea kuanzia kiangazi kijacho.

Tayari kocha huyo alishatangaza kwamba ataachia nafasi yake nchini
Italia baada ya michuano ya Euro 2016 na aliwasili jijini London
Jumapili mchana; maelezo yasiyo rasmi yakiwa kwamba anasaini mkataba
wa miaka mitatu Stamford Bridge kuanzia msimu ujao.

Chelsea wamekuwa wakitafuta kocha wa kudumu tangu kufukuzwa kazi kwa
Jose Mourinho, ambapo bosi wa mpito, Guus Hiddink anaelekea
kukamilisha kazi yake mwishoni mwa msimu, ikiwa ni mara ya pili
anaitwa kuokoa jahazi lililokuwa likizama na alishasema hangekaa zaidi
ya mwisho wa msimu hapo.

Wawakilishi wa Conte mwenye umri wa miaka 46 walianza majadiliano na
Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia tangu Februari. Conte
ametwaa ubingwa wa Italia – Serie A akiwa na Juventus mara tatu kabla
ya kujiuzulu 2014, kisha akawaongoza Timu ya Taifa ya Italia – Azzurri
kufuzu fainali za Euro zinazofanyika Ufaransa kiangazi kijacho.

Ilitangazwa mwezi uliopita kwamba Conte alikuwa anataka kurudi katika
kufundisha klabu na si timu za taifa, hivyo angeachia ngazi Azzurri
mara baada ya fainali hizo. Mourinho alipata kusema kwamba kufundisha
timu ya taifa ni kazi ya wazee.

Kocha Hiddink ametoa rai kwa mrithi wake yeyote awaye kuzingatia
matumizi ya vijana kama msingi wa mafanikio kwa timu hiyo,akisema kuna
vipaji vingi vinavyotakiwa kukuzwa na kutumiwa, badala ya kutumia
vijeba.

Timu ya Taifa ya Syria wanataka kumwajiri Mourinho kuwa kocha wao,
lakini kuna wasiwasi iwapo ataikubali nafasi hiyo, ikizingatiwa hali
ya kisiasa na kijamii ya Syria ilivyo tete. Valencia wa Hispania pia
wanaelezwa kutaka huduma za kocha huyo, baada ya kumfuta kazi Gary
Neville.

Katika hatua nyingine, mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG)
wametoa ofa ya kumchukua mshambuliaji wa Kihispania asiyetulia wa
Chelsea, Diego Costa, 27 kuwatumikia msimu ujao.

Golikipa wa zamani wa Manchester United,Peter Schmeichel anaamini
kwamba nahodha wa klabu hiyo, Wayne Rooney anatakiwa kuondoshwa kwenye
eneo la ushambuliaji na badala yake awe kiungo wa timu hiyo.

Rooney, 30, anasisitiza kwamba bado ana miaka michache ya kucheza kama
mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya England – Three Lions, ambapo kocha
Roy Hodgson amesisitiza kwamba ndiye ataongoza wenzake kwenye Euro
2016.

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano na Benfica kwa ajili
ya kumsajili kiungo wao, Renato Sanches kwa pauni milioni 40.

Kocha wa West Ham, Slaven Bilic amesema amechoshwa na kuomba wachezaji
wake wasipewe kadi nyekundu, kutokana na kukithiri kuadhibiwa kwa
wachezaji hao, ambapo wikiendi hii Cheikhou Kouyate alitolewa nje
walipokwenda sare ya 2-2 na Crystal Palace.

Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon amedai kwamba klabu hiyo
wamekubaliana na Manchester United kumchukua kipa David De Gea, 25.
Alitarajiwa kuhamia Madrid msimu ujao, lakini mchakato wa dakika za
mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa ukakwama.

Mshambuliaji anayetakiwa na Chelsea, Edison Cavani, 29, atafanya
mazungumzo na klabu yake – PSG kwani raia huyo wa Uruguay anataka
kujua hatima yake, muda atakaopewa kucheza na ikibidi aondoke. Zlatan
Ibrahimovic ndiye hupewa kipaumbele na mabingwa hao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Leicester hawakamatiki

Tanzania Sports

Rooney Hahitajiki Kwenye Kikosi cha England?!