in , , , ,

Christian Benitez: Dharau katika kifo


*Wahusisha kifo na Kombe la Dunia Qatar

Kifo cha mshambuliaji wa kimataifa wa Ecuador, Christian Benitez kimeshitua wengi, huku dunia ikikerwa na upotoshaji wa jinsi mauti yalivyomkuta.
Katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia, mitandao ya jamii ndiyo ilitumika kutangaza habari za kifo hicho.
Kwa upotoshaji mkubwa, ilielezwa kwamba Benitez alikufa katika ajali ya gari nchini Qatar, wakati alifariki hospitalini baada ya kuhisi maumivu makali tumboni.
Mbaya zaidi, ni kwamba kuna vyombo vya habari vilidaka habari hiyo juu juu, na kuihusisha na kampeni za kuhamisha uenyeji wa Kombe la Dunia kutoka Qatar 2022.
Katika muktadha wa kwanza, iliripotiwa kwamba Benitez (27) aliyepata kuchezea Birmingham City ya Uingereza alifariki kwa ajali ya gari.
Yaelekea kulikuwa na hila katika mlengo huo, ikilengwa kuonesha kwamba alikufa baada ya kukuka sheria za barabarani na kuendesha kwa kasi kupita kiasi.
Qatar inajulikana kwa uchache wa ajali za barabarani, kutokana na mfumo mzuri wa udhibiti wa uendeshaji vyombo vya moto, na nidhamu iliyojengeka kwa ujumla.
Pengine walitaka kuonesha kwamba ama hakuna barabara nzuri, au kwamba kuna sheria mbovu na usimamizi usiofaa na hivyo ingekuwa hatari kwa wageni wakati wa mashindano hayo makubwa zaidi ya soka duniani.
Lakini, katika hatua nyingine, kuna vyombo vilivyoripoti kwamba kijana huyo alifariki dunia baada ya kucheza kwenye hali ya joto kali, katika miezi ya Julai/Agosti kama itakavyokuwa kwenye michuano hiyo.
Propaganda hizo zinalenga kuwatisha wachezaji na wadau wengine wa soka, kwamba kuna uwezekano mkubwa wa wachezaji watakaoshiriki ama kufariki dunia au kuugua kutokana na joto kali litakalotawala wakati huo.
Wahusika kwenye mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook, walisambaza habari za aina ya kifo hicho, isivyokuwa sawa, mithili ya mpuliza filimbi wa Hamelin.
Ukweli ni kwamba, Benitez alifariki kutokana na maradhi yanayohusishwa na moyo na pia kushindwa kupumua, saa chache baada ya kuchezea klabu yake mpya ya El Jaish ya Qatar.
Chama cha Soka cha Ecuador kilitangaza kifo chake baadaye na kutuma salamu za rambirambi, kikisema baada ya kulalamikia maumivu makali tumboni, alipelekwa hospitali, lakini madaktari hawakuweza kuokoa maisha yake.
Qatar imeshachaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2022 lakini kuna malalamiko kwamba kwa wakati wa kiangazi, joto litakuwa kali mno.
Wachambuzi wa mambo wanasema inawezekana kucheza baada ya Jua kutua, huku wadau wakitakiwa kunywa maji kwa wingi, lakini pia wanasema hayatanoga sana kwa wachezaji miezi hiyo ya Julai na Agosti wala kwa washabiki.
Iwe iwavyo, suala la uenyeji wa Qatar katika miezi hiyo, kuhamishia nyakati za majira ya baridi au kuiondosha Qatar kabisa, haikutakiwa kuhusishwa katika habari za kifo cha Benitez.
Kifo cha mwanasoka huyu mahiri aliyefunga mabao mazuri kwa klabu na taifa lake, kilitakiwa kutangazwa kwa heshima zaidi na takwimu zote kuwa sahihi tangu mwanzo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wazazi wa Gareth Bale waingilia usajili

*USAJILI WA WACHEZAJI SASA MWISHO AGOSTI 5*