in , , ,

Chelsea wapigwa tena

 

*Arsenal wachanua, Man City safi

*Man United wawafyatua Liverpool

Ligi Kuu ya England (EPL) imeingia mzunguko wa tano kwa matokeo ya kushitua, ambapo Chelsea wamepoteza mechi ya tatu kati ya tano walizocheza.

Chelsea wanaofundishwa na Jose Mourinho wametandikwa 3-1 na Everton, huku Steven Naismith akifunga mabao yote kwa Everton.

Naismith aliingia kuchukua nafasi ya Muhamed Besic aliyeumia mapema kipindi cha kwanza na hakuchukua muda mrefu kufunga mabao mawili.

Chelsea walijibu kupitia kwa Nemanja Matic aliyefunga kwa shuti la mita 30 lakini Naismith tena alitikisa nyavu za Chelsea, ambao langoni alikuwapo Asmir Begovic

Hii ni mara ya kwanza tangu 1986 kwa Chelsea kufanya vibaya kiasi hiki kwenye mechi tano za awali kwenye msimu, ambapo kati ya pointi 15 ambazo wangeweza kukusanya, wamepata nne tu na sasa wapo nafasi ya 16.

Hata hivyo, Mourinho ameeleza kutokuwa na wasiwasi na hali hiyo, akisema hahisi shinikizo lolote na kwamba yeye ndiye mtu sahihi bado wa kufundisha timu hiyo, kwani hakuna anayeweza kuleta mafanikio zaidi yake.

Amesema si sahihi kuangalia jedwali la msimamo wa ligi kwa sasa na kwamba yeye anawatazama wachezaji, kwenye mazoezi na kujipima kwa mechi zinazokuja na si jedwali.

Chelsea walikabiliana na mlinzi ambaye walikuwa wakitaka kumsajili, John Stones, aliyeomba kuondoka Everton lakini akakataliwa, na kuna habari pia kwamba siku ya mwisho ya msimu walitoa ofa kumsajili mlinzi Marquinhos wa Paris Saint-Germain (PSG).

Katika beki ya kati, Mourinho aliwatumia Kurt Zouma na nahodha John Terry aliyerejea baada ya kutumikia adhabu moja kwa kadi nyekundu.
Gary Cahill aliachwa benchi wakati John Mikel Obi aliitwa kucheza na Matic lakini mambo hayakuwa mazuri. Cesc Fabregas, Eden Hazard na Diego Costa nao walionekana kuwa chini kiviwango.

ARSENAL WAWAZIDI NGUVU STOKE

AS
Arsenal wamepata ushindi wa kwanza wa msimu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Emirates, kwa mabao ya Theo Walcott na Olivier Giroud dhidi ya Stoke.

Walcott ndiye alifungua kitabu cha mabao katika kipindi cha kwanza, akikimbilia vyema mpira mrefu wa Mesut Ozil kabla ya kumzidi nguvu kipa Jack Butland.

Giroud aliyeingia kipindi cha pili alifunga bao kuhakikisha ushindi dhidi ya Stoke ambao hawajapata kushinda kwenye uwanja wa wapinzani wao hao tangu 1981.

MAN CITY USHINDI 100%

sa
Manchester City wameendeleza ushindi kwa asilimia 100 kwenye msimu huu, walipowashinda

Crystal Palace 1-0 kwa bao la dakika za majeruhi.

Alikuwa ni Mnigeria, Kelechi Iheanacho aliyefunga bao hilo, likiwa la kwanza kwake tangu ajiunge na timu ya wakubwa, baada ya kupata mpira wa Samir Nasri ulioparazwa na kipa wa Palace.

Man City walipata pigo kwani mshambuliaji wao mahiri, Sergio Aguero aliumia goti ikiwa ni siku tatu kabla ya kupambana na Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Ni hapo walimwingiza mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili msimu huu, Kevin de Bruyne huku makocha Manuel Pellegrini na Alan Pardew wakivutana juu ya tukio la kuumizwa kwa Aguero na mlinzi wa Palace, Scott Dann aliyepewa kadi ya njano.

UNITED WAWAZIDI LIVERPOOL MAARIFA

martial
Manchester United wakicheza nyumbani wamewazidi nguvu Liverpool kwa kuwafunga 3-1.

Mabao ya United yalifungwa na Daley Blind, Andre Herrera kwa penati na mchezaji wao mpya, Anthony Martial.

Liverpool ambao hawajawa vyema sana msimu huu walipata bao lao kupitia kwa Christian Benteke.

Katika mechi nyingine, Norwich waliwafunga Bournemouth 3-1, Watford wakawazidi akili Swansea kwa kuwapiga 1-0 na West Bromwich Albion wakienda suluhu na Southampton.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Van Gaal: Mimi si dikteta

Tanzania Sports

Leicester wawafunga Villa