in , , ,

Chelsea wamfukuza Mourinho

Hatimaye Chelsea wamemfukuza kocha wao, Jose Mourinho aliyependa
kujiita majina ya ajabu kama The Special One, The Only One au The
Happy One.

Hatua hiyo imechukuliwa na mmiliki wa klabu, bilionea wa Urusi, Roman
Abramovich, sababu ikiwa mwenendo mbovu kwenye Ligi Kuu, ambapo
Chelsea wapo nafasi ya 16 baada ya mechi 16 pia wakiwa na pointi 15.

Chelsea waliopoteza matumaini ya kutetea ubingwa huo kutokana na
tofauti ya pointi 20 iliyopo kati yao na vinara Leicester wameondokana
na kocha aliyewaongoza wka mafanikio makubwa na kutwaa ubingwa miezi
saba tu iliyopita.

Mourinho (52) alirejea Chelsea Juni 2013 kwa awamu ya pili, ambapo
msimu uliopita walimaliza ligi wakiwaacha waliowafuatia, Manchester
City kwa tofauti ya pointi nane. Mechi yake ya mwisho ilikuwa Jumatatu
wiki hii ambapo walichapwa 2-1 na Leicester.

Taarifa ya Klabu ya Chelsea iliyotolewa muda mfupi uliopita imedai
kwamba wameamua kuachana kwa maridhiano.

“Wote katika Chelsea tunamshukuru Jose kwa mchango wake mkubwa tangu
aliporejea kama kocha kiangazi cha 2013. Makombe yake matatu ya
ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ngao ya Hisani pamoja na makombe
matatu ya Kombe la Ligi katika misimu miwili vinamfanya kuwa kocha
aliyefanikiwa zaidi katika historia yetu ya miaka 110.

“Lakini Jose na bodi wamekubaliana kwamba matokeo si mazuri msimu huu
na wanaamini kwamba kilicho bora kwa kila upande ni kuachana. Klabu
wanapenda kuweka wazi kwamba Jose anaondoka kukiwa na uhusiano mzuri
na atabaki mtu aliyependwa sana, kuheshimiwa na muhimu kwa Chelsea.

“Ameacha alama kubwa Stamford Bridge na England na siku zote
anakaribishwa Stamford Bridge. Klabu sasa inajielekeza kuhakikisha
kwamba kikosi chetu chenye vipaji vingi kinafika pale panapotakiwa.
Hatutazungumzia suala hili tena hadi uteuzi wa kocha mpya
utakapofanywa,” ilisomeka taarifa ya Chelsea.

Kumbukumbu ya utendaji kazi wa Jose
Kumbukumbu ya utendaji kazi wa Jose

Mhariri wa Michezo wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Dan Roan anasema:

“Jose Mourinho alikuwa na mkutano klabuni kuanzia saa 8:30 (saa 11:30
kwa saa za Afrika Mashariki) na ndipo akaambiwa mwisho wake umefika.
Ameachiwa kuondoka baada ya kipindi chake cha pili klabuni na
hatalipwa fidia ya pauni milioni 40 zilizokuwa zikitajwa kwenye
tetesi. Ninachoelewa ni kwamba alishapewa malipo ya hadi mwisho wa
msimu na kilichobaki ni pauni milioni 12.

“Wakati hakuna ubishi kwamba amepata mafanikio makubwa Ulaya,
ameshindwa kusimamia timu na kupata matokeo mazuri kwa kipindi kirefu.
Chelsea (Bodi) walikabiliwa na shida katika kufanya uamuzi ndipo Roman
Abramovich akautoa.”

Baada ya kuondoka kwake, anatarajiwa kutafutwa kocha wa muda au wa
kudumu na majina yanayotajwa kwa kudumu ni Pep Guardiola wa Bayern
Munich na Diego Simeone wa Atletico Madrid wakati wale wa muda
wanaotajwa ni Brendan Rodgers aliyefukuzwa Liverpool majuzi, Guus
Hiddink aliyepata kufundisha hapo Stamford Bridge au Juande Ramos.

Anaondoka wakati vyombo vya habari vikiwa vimemkatia jina la The
Unhappy One, akiwaacha Chelsea wakiwa pointi moja tu juu ya mstari wa
kushuka daraja huku akiwa ameshasema uwezekano wa kutwaa ubingwa wala
wa kushika nafasi nne za juu haupo na sasa wanapigana ili wanusurike
kushuka daraja.

Mourinho alisaini mkataba mpya wa miaka minne klabuni hapo Agosti 7
mwaka huu na ndiye kocha aliyepata mafanikio makubwa zaidi hapo,
akitwaa ubingwa wa England mara tatu. Alinukuliwa juzi akisema alihisi
kuwapo usaliti miongoni mwa wachezaji kwa kazi kubwa aliyofanya kuwapa
viwango vya juu kimchezo na kwamba alitakiwa kuuza baadhi yao kiangazi
kilichopita.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mourinho ajadiliwa Chelsea

Tanzania Sports

Uswisi wakamata mamilioni ya FIFA