in , , ,

Chelsea wabweteka wabanwa

Chelsea wamepoteza pointi mbili muhimu katika mechi dhidi ya West Bromwich Albion na tatizo lao ni kubweteka kwa kuwa juu.

Timu zote zilianza mchezo vyema, huku West Brom waliokuwa katika nafasi ya kushuka daraja ikitandaza soka safi kana kwamba haipo huko.

Baada ya kuwabana Chelsea kwa dakika 45 hivi, Branislav Ivanovic aliwafungia Chelsea baada ya mabeki wa Baggies kuzembea kufagia mpira wa kona ya pili, sekunde nane kabla ya mapumziko.

Hali hiyo iliwafanya vijana wa Jose Mourinho kurudi uwanjani wakiwa na kibri, lakini mara walianza kupoteana na wale wa kocha mpya Pepe Mel kuanza kuwashambulia kwa nguvu.

Mel alibadilisha wachezaji watatu katika muda mfupi kwenye mchezo huo ambao kadi za njano zilitawala, hasa robo ya pili ya kipindi hicho, Chelsea wakilamba kadi nne kwa kuwakwatua Baggies ili wasifunge.

Hata hivyo alikuwa Victor Anichebe aliyeingia dakika ya 73 aliyefunga kusawazisha bao dakika ya 87 na kuacha Chelsea wakiwa hawaamini kuwa wanatoka 1-1.

Kuona hivyo Mourinho aliyetaka kumwingiza Frank Lampard alibadilisha na kumwingiza mshambuliaji matata wa Misri aliyetoka FC Basel ya Uswisi.

Mohammed Salah badala ya Samuel Eto’o ambaye hakung’ara lakini hawakuweza kurejesha pointi mbili walizopokonywa.

Hata hivyo, Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya pointi mbili baada ya kujikusanyia pointi 57, wakisubiri kwa hamu matokeo ya mechi ya Jumatano hii baina ya wanaowafuata, Arsenal dhidi ya Manchester United katika dimba la Emarati.

WEST HAM, SAINTS WAPATA POINTI TATU

Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku wa Jumanne, West Ham walipata pointi mbili muhimu baada ya kuwafunga Norwich 2-0 na kutoka maeneo ya hatari ya kushuka daraja hadi nafasi ya 10.

Hull walizama nyumbani kwa kufungwa na Southampton 1-0 wakati Cardiff walikwenda suluhu na Aston Villa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Nahodha wa England ni msagaji

TWIGA STARS IKO VIZURI KUIVAA ZAMBIA- KOCHA