in , ,

Chelsea mabingwa Kombe la Ligi

Kocha Mreno, Jose Mourinho ametwaa kombe la kwanza tangu kurejea Chelsea kwa mara ya pili.
Chelsea wametwaa ubingwa kwenye fainali ya Kombe la Ligi, linalojulikana zaidi kama Capital One Cup iliyofanyika kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Tottenham Hotspur.
Alikuwa nahodha John Terry na mshambuliaji wa kati wa Hispania, Diego Costa waliowaharibu Spurs, mabao yote yakisaidiwa na mparazo, moja kila kipindi.

Ilikuwa mechi ya kihistoria, kwani miaka saba iliyopita Spurs waliwashinda Chelsea na kutwaa ubingwa kwenye mashindano kama haya na Januari mosi mwaka huu Spurs waliwatandika Chelsea 5-3 walipocheza White Hart Lane.

Hiki ni kikombe cha kwanza kwa Mounriho tangu alipotwaa ubingwa wa La Liga nchini Hispania akiwa na Real Madrid 2012 wakati kwa Chelsea ni cha kwanza tangu walipotwaa ubingwa wa Ligi ya Europa mwaka mmoja baadaye walipowashinda Benfica jijini Amsterdam, Uholanzi.

Licha ya kuwa haya ni mashindano madogo zaidi kwa timu kubwa za hapa na kwamba Mourinho alishatwaa makombe mengi, amedai kuwa hii ilikuwa fainali muhimu zaidi kwake.
Mourinho alimpanga beki wa kati, Kurt Zouma kucheza kwenye kiungo kuziba pengo lililoachwa na Nemanja Matic ambaye amezuiwa kucheza kwa sababu ya kadi.

Spurs, licha ya washabiki wake kuwa na hamu ya kurudia historia, dimbani hawakuonekana kukaribia kufanya hivyo, ndipo shuti la kwanza la Chelsea lililolenga goli likatinga wavuni.
Spurs wanaofundishwa na Mouricio Pochettino ndio kwanza wametolewa kwenye Ligi ya Europa walipofungwa na Fiorentina wa Italia Alhamisi iliyopita lakini walishindwa kumtungua Petr Cech aliyerejeshwa langoni badala ya chaguo la kwanza, Thibaut Courtois.

Costa alikuwa mwimba kwa Spurs, akitunishiana misuli na wachezaji wao, ambapo alifika mahali wakakasirikiana na Nabil Bentaleb, Kyle Walker na Eric Dier katika matukio tofauti. Aliwazidi nguvu, hata hivyo, na kufunga bao lake la 17 msimu huu, japokuwa halikuhesabiwa kwake bali kwa mchezaji wa Spurs kama bao la kujifunga.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Liverpool wawafunga Man City

EPL yafika patamu