in , , ,

‘Chelsea jitazameni kwenye kioo’

*Hiddink awaambia wajiandae upya

Kocha wa mpito wa Chelsea, Guus Hiddink amewaambia wachezaji wake
kwamba wanatakiwa kujitafakari upya, kutafuta kioo na kujiangalia kwa
muda mrefu kisha kuhakikisha wanajituma kuiokoa klabu inayozama.

Raia huyu wa Uholanzi amewaambia wanahabari kwenye mkutano wake wa
kwanza tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo kwamba klabu ipo katika
wakati mgumu na ameshawaeleza kila kitu wachezaji wake.

Hiddink anasema kwamba amewaaambia wajitazame kwenye kioo, si mara
moja wala mbili, bali mara nyingi na kisha wahakikishe wanajiandaa
upya kwa kazi nzito iliyo mbele yao, akisema kwamba kurejea kwake
Stamford Bridge si hakikisho kwamba watafanikiwa.

“Nimezungumza na kikosi changu; tulizungumza kidogo juu ya mambo
yaliyopita … wakati nikiwa hapa, sababu za sie kuwa chini hivi. Lakini
pia niliwaambia mambo haya hutokea kwenye soka na nataka kila mmoja
kujitazama kwenye kioo, si mara moja au mbili tu bali kwa muda mrefu,”
akasema kocha huyo anayerejewa kama ‘mtatua matatizo.

Cesc Fàbregas
Cesc Fàbregas

Hiddink (69) aliyechukua nafasi ya Jose Mourinho aliyefutwa kazi,
alipata kufanya kazi klabuni hapo kwa mpito pia msimu wa 2008/2009
baada ya mmiliki Roman Abramovich kumfukuza kocha Luiz Felipe Scolari
na safari hii pia atahudumu hadi mwisho wa msimu.

Mdachi huyu anasema atawaweka kitako wachezaji kadhaa wanaoonesha
kutokuwa katika hali nzuri kisoka ili kuona wanafanyaje na pia
amezungumza uwezekano wa kuwa na Didier Drogba kwenye benchi lake la
ufundi, japo anasema hajui iwapo mchakato huo utawezekana.

Chelsea wapo nafasi ya 15 katika Ligi Kuu ya England baada ya kucheza
mechi 17, wakiwa na pointi tatu tu juu ya mstari wa kushuka daraja.
Hiddink amesema kihesabu bado wanaweza kumaliza ligi katika nafasi nne
za juu, lakini akakiri kwamba itakuwa kazi ngumu.

“Ligi hii ni ngumu sana, kila timu inaweza kuua nyingine. Si kitu cha
kawaida mie kuingia hapa katikati ya msimu. Ina maana mambo hayaendi
sawa. Lakini, iwe iwavyo, nafurahi kurejea hapa, ni miaka michache
iliyopita nilikuwa hapa katika mazingira haya haya.

“Si rahisi baada ya kuwa mmetwaa ubingwa maana mnabweteka baada ya
kujisahau hadi mje kushituliwa mambo yakishaharibika. Si rahisi kusema
kwamba eti madhali nimekuja basi tatizo limemalizika,” anasema.

Akimzungumzia kocha Mourinho aliyetimuliwa na anayehusishwa na
Manchester United, Hiddink anasema: “Ukitazama rekodi yake kwa miaka
yote hiyo ni nzuri sana, alizoa mataji mengi tu. Hata hivyo mambo haya
hutokea kwenye soka. Watu huchukua uamuzi kama walivyofanya sasa nami
huja ninapoombwa.”

Alipoulizwa iwapo Januari atasajili wachezaji zaidi, alisema angependa
kwanza apewe muda katika mechi chache zinazokuja kisha ataona cha
kufanya. Akaongeza kwamba anatarajia washabiki wataiunga mkono timu
kama walivyofanya kipindi chake kilichopita ambapo alitwaa Kombe la
FA.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Van Gaal awekwa mtu kati

Tanzania Sports

Kizungumkuti Ligi Kuu