in , , ,

Benteke kumbadili Sturridge Liverpool?

 

*Man United watatumia pauni milioni 200

*Chelsea wataka £10m kumuuza Petr Cech

 

Wakala wa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, amesema kwamba ana uhakika wa asilimia 90 kwamba raia huyo wa ivory Coast ataondoka kiangazi hiki.

 

Wakala huyo, Dimitri Seluk amesema kwamba kuna klabu tatu zinazomtaka mchezaji huyo bora wa Afrika, lakini atafanya uamuzi wa pa kwenda msimu ukishamalizika.

 

Ripoti zinaonesha kwamba Inter Milan na Paris Saint-Germain (PSG) ni kati ya klabu zinazomhitaji Toure (31) ambaye msimu huu hakuwa na kiwango cha juu na City wakapoteza ubingwa kwa Chelsea.

 

Seluk amethibitisha kwamba yupo jijini London na anatarajia kukutana na City kwa ajili ya kujadili hatima ya kiungo huyo, lakini hakuna tarehe iliyopangwa kwa mazungumzo hayo.

 

Ameiambia Sky Sports News: “Uhakika wa yeye kuondoka Manchester United kiangazi hiki ni asilimia 90. Tunasubiri hadi mwisho wa msimu kufanya hivyo.”

 

Toure ana miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wake kuhudumu City, kwani aliuhuisha 2013 kwa miaka minne. Aliingia Etihad 2010 akitoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 24.

 

Toure analipwa mshahara mkubwa wa pauni 220,000 kwa wiki ambao City wanaona ni mkubwa mno ikilinganishwa na kiwango na mchango wake kwa timu na klabu.

 

Seluk amesema ni wakati mwafaka sasa kwa Toure kuondoka kutafuta maisha sehemu nyingine. Amecheza hapo mechi zaidi ya 200 na kufunga mabao 62 katika michuano yote.

Mwaka jana wakati kama huu, kulikuwa na sintofahamu juu ya hatima ya Toure, baada ya mwenyewe kukosa raha Etihad kwa vile hakupewa zawadi ya siku ya kuzaliwa na viongozi wala wamiliki wa City.

 

Siku yake ya kuzaliwa ikiwa inakaribia, Mei 13, Seluk alisema kwa kutania: “Nimekuja London kumletea Yaya keki ya siku yake ya kuzaliwa na kuhakikisha kwamba Manchester City wanamnunulia keki kadhalika.”

 

Yapo maelezo kwamba ikiwa City wanataka sana kuondoka kwa Toure ili kuepuka mshahara huo mkubwa, upo uwezekano wakamtoa bure

 

Sturridge nje, Liverpool wamwinda Benteke 

Kijana huyu amekuwa akikumbwa na maumivu ya goti kwa muda sasa
Kijana huyu amekuwa akikumbwa na maumivu ya goti kwa muda sasa

 

Mshambuliaji wa kati wa Liverpool aliyefanyiwa upasuaji wa paja, Daniel Sturridge atakuwa nje ya dimba kwa miezi mitano, hivyo klabu wanatafuta mshambuliaji mkali.

 

Brendan Rodgers anadaiwa kufikiria kumsajili mpachika mabao wa Aston Villa, Christian Benteke.

 

Msimu huu ulianza vibaya kwa Liver bila ya Luis Suarez aliyeuzwa Barcelona, na ujao watamkosa Sturridge hadi Septemba, akiwa ndiye tegemeo lao kubwa.

 

Rodgers amepata kusema pia kwamba lazima mchezaji huyo apande kiwango na kuwathibitishia kwamba anaweza kuwapo Anfield kwa uendelevu.

 

Benteke (24) naye alitoka kuumia, akawa chini ya kiwango kwa muda, lakini sasa kocha mpya, Tim Sherwood amefufua makali yake.

 

Manchester City wanaingia vitani na wapinzani wao, Chelsea na Arsenal kumuwania kiungo wa Hoffenheim, Roberto Firmino, 23, kutoka Brazil, anayethaminishwa kwa pauni milioni 20.

 

Manchester United wanasemekana wamempatia kocha Louis van Gaal pauni milioni 200 kwa ajili ya usajili, ambapo mkali zaidi anayetafutwa ni Gareth Bale wa Real Madrid.

 

Hata hivyo, wakala wa Bale, Jonathan Barnett amedai kwamba Mwingereza huyo hataondoka Madrid.

 

Baada ya kukubaliwa kumsajili Memphis Depay kutoka PSV Eindhoiven, Bale, 25, anawindwa sambamba na mlinzi wa Borussia Dortmund, Mats Hummels na beki wa kulia, Nathaniel Clyne, 24, wa Southampton.

 

Habari za karibuni zinasema kwamba Radamel Falcao, 29, anatarajiwa kuondoka Old Trafford baada ya msimu wa mkopo ambao umekuwa hovyo kwake.

 

AC Milan watakuwa tayari kumchukua raia huyu wa Colombia na kumpa nafasi ya kuumba upya maisha yake ya muziki. Haijulikani ikiwa klabu yake ya Monaco haimhitaji.

 

Darren Bent anatarajiwa kurejea Aston Villa kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kocha mpya, Tim Sherwood kusema anataka kumchukua tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.

 

Chelsea wanasema kwamba watahitaji pauni milioni 10 ikiwa Arsenal wanamtaka kipa wao,

Petr Cech, 32, japokuwa kipa huyo amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

 

Liverpool watachuana na Manchester City na Bayern Munich kumpata mchezaji mwenye umri wa miaka 22 wa Lazio, Felipe Anderson anayekadiriwa kuwa na pauni milioni 30.

 

Beki wa kulia wa Tottenham Hotspur, Danny Rose, 24, anatakiwa na Atletico Madrid na Manchester City.

 

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amechukua hatua isiyo ya kawaida ya kuwapa wachezaji wake mapumziko ya siku nne wiki hii kabla ya mechi yao dhidi ya Liverpool Jumapili hii.

Golikipa mzoeefu, na watu wengi wanaamini, umri unapokuwa mkubwa, ndipo unadaka vizuri
Golikipa mzoeefu, na watu wengi wanaamini, umri unapokuwa mkubwa, ndipo unadaka vizuri

 

Uamuzi huo umewashtua Manchester United wanaopigana kumbo la Liverpool kuwania nafasi ya tatu za juu ili kufuzu kucheza ligi ya Ulaya.

 

Kocha wa muda wa Newcastle, John Carver anasema kwamba angekuwa amefukuzwa na klabu nyingi za Ligi Kuu kama angekuwa kwao na kufungwa mechi nane mfululizo.

 

Carver anasema kwamba Newcastle ni tofauti na sasa anaungwa mkono kwa asilimia 100 na mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Kimbunga cha kushuka daraja EPL

Manchester United waamka