in , , ,

BAYERN MUNICH SI KIKWAZO KWA ARSENAL

 

Arsenal wamepangwa kundi moja na Bayern Munich kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu utakaoanza Septemba 15 mwaka huu. Kwenye kundi hilo (Kundi F) pia wamo Olympiakos kutoka Ugiriki na Dinamo Zagreb wa Croatia.

 

Washabiki wengi wa soka wanadhani kwamba makali ya Bayern Munich ni kikwazo mno kwa Arsenal na huenda Washika Bunduki hao wa London watashindwa kuvuka hatua za makundi.

 

Hata washabiki wa Arsenal hawajafurahishwa kuona timu yao imo kwenye kundi moja na Bayern ambao ni moja kati ya timu tishio za Ulaya kwa sasa. Nadhani ni kwa sababu timu yao imeondolewa na wababe hawa mara mbili kwenye michuano hii ya Ulaya ndani ya misimu mitatu iliyopita.

 

Mchezaji wa zamani wa Bayern Owen Hargreaves amesema kuwa ana uhakika Arsenal hawawezi kuwa vinara wa kundi hili. Jerome Boateng ameonyesha kufurahia kuwemo kwenye kundi moja na Arsenal. Mlinzi huyo wa Bayern amesema kuwa wao huwa wanakuwa na wakati mzuri mno wanapocheza na Arsenal.

advertisement
Advertisement

 

Hata hivyo kwa upande wangu sidhani kwamba Arsenal wana nia ya kusaka kuwa vinara wa kundi hili. Kocha wao na wachezaji wenyewe wanajua wazi kuwa hilo ni swala gumu kwao. Nafikiri kitu pekee watakachopigania ni kuhakikisha wanafuzu na kuingia kwenye hatua za 16 bora.

 

Kimsingi wanao uwezo wa kukusanya alama za kutosha kuwaweka kwenye nafasi mbili za juu. Naungana na kiungo wa Bayern Thiago Alcantara ambaye amesema kuwa itakuwa ni jambo la kushangaza iwapo Arsenal au Bayern itashindwa kuvuka hatua za makundi.

 

Ikumbukwe kwenye michezo minne iliyopita baina ya timu hizi Arsenal waliweza kushinda mchezo mmoja kwa 2-0 kule Allianz Arena Ujerumani Machi 2013 na wakaweza kutoa sare ya 1-1 kwenye dimba hilo hilo Machi 2014. Bayern walipata ushindi mara mbili tu kwenye michezo hiyo minne.

 

Hivyo ni wazi kuwa ingawa Bayern wanawazidi Arsenal kiuwezo haitakuwa jambo rahisi kwao kuchukua alama zote sita dhidi ya timu hiyo. Kuna uwezekano mkubwa timu hizi zikagawana alama ama 3 kwa 3 ama Arsenal wakachukua alama moja. Lolote litakalotokea kati ya hayo litakuwa si jambo baya kwa Arsenal.

 

Pia ikumbkwe kuwa hata Olympiakos na Zagreb nao watapoteza alama watakapokutana na Bayern. Kuna uwezekano Bayern wakazipiga nyumbani na ugenini timu mbili hizi. Hili litakuwa jambo zuri kwa Arsenal kwani nafasi yake ya pili itakuwa mahala salama.

 

Zaidi ya hapo ikumbukwe kuwa Arsenal pia ina uwezo wa kuwaadhibu Olympiakos na Zagreb na kujiweka kwenye nafasi nzuri. Dinamo Zagreb pengine ndio timu dhaifu kuliko timu zote kwenye kundi hili.

 

Mara ya mwisho kushiriki Ligi ya Mabingwa ilikuwa msimu wa 2012/13 na wakapoteza michezo mitano kati ya sita ya Kundi A na kutoa sare moja. Sitarajii kuona Arsenal wakishindwa kuifunga timu hii kwenye michezo yote miwili.

 

Pengine kwenye michezo dhidi ya Olympiakos ndipo Wenger na kikosi wanapotakiwa kuelekeza akili zao na nguvu zaidi ili wahakikishe wanawafunga vijana hawa wa Ugiriki michezo yote miwili.

 

Kwenye msimu wa 2012/13 Arsenal na Olympiakos walikuwemo kwenye kundi moja. Arsenal waliwafunga Olympiakos 3-1 wakiwa nyumbani na Olympiakos wakashinda 2-1 kwao Ugiriki.

 

Hivyo nadhani Olympiakos ndiyo wanaweza kuwa kikwazo kwa Arsenal kwenye malengo yao ya kuvuka hatua za makundi. Arsenal hawatakiwi kuwaruhusu hawa jamaa kujipatia alama kwenye michezo watakayokutana nao.

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

UBINGWA WA RIADHA DUNIANI:

Tanzania Sports

Arsenal ushindi mwembamba