in , , ,

Bayern, Barcelona wapeta UCL

 

Bayern Munich na Barcelona wametinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuwafyatua wapinzani wao.

 

Wakitoka kufungwa 3-1 na Porto, Bayern waliingia uwanjani nyumbani kwao kwa nguvu na kufanikiwa kushinda 6-1.

 

Kocha Pep Guardiola alishasema mapema kwamba kufungwao kwenye mechi ya kwanza hakukumsumbua sana na aliridhishwa na mazoezi ya kujiandaa na mechi ya mkondo wa pili.

 

Hii ni mara ya nne mfululizo kwa Bayern kufika nusu fainali, ambapo mwaka huu wamevuka kwa ulinganifu wa mabao 7-4.

 

Iliwachukua dakika 27 kufuta mabao mawili waliyokuwa wakidaiwa, ambapo Porto walikuwa hoi katika kipindi cha kwanza.

 

Bayern walikuwa wakihitaji walau ushindi wa 2-0 ambapo wangefaidika na bao la ugenini, na walipata mabao hayo kupitia kwa Thiago

Alcantara na Jerome Boateng, wote wakifunga kwa vichwa.

 

Robert Lewandowksi aliendeleza maumivu kwa Porto kwa kufunga la tatu kabla ya Thomas Muller kufunga la nne.

 

Lewandowski alizifumania nyavu kwa mara ya pili kabla ya Jackson Martinez kuwapa Porto matumaini kwa kufunga bao. Hata hivyo, Porto walipata pigo kwa Ivan Marcano kutolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya, ambapo Xabi Alonso alitia msumari wa mwisho kwenye jeneza kwa kufunga kwa mpira wa adhabu.

 

Matokeo haya yanamfanya Guardiola kufika nusu fainali ya michuano hiyo kwa misimu yote sita aliyokuwa kocha.

 

Tangu achukue mikoba ya ukocha Bayern kutoka kwa Jupp Heynckes 2013, Bavaria hao wamepoteza mechi nne tu kati ya 63 walizocheza.

 

 

 

BARCELONA WAWATUPA NJE PSG

Neymar

 

Barcelona wameendeleza ubabe kwa Paris Saint-Germain (PSG) kwa kuwatungua 2-0, baada ya kuwatuliza pia kwa 3-1 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Neymar ndiye alikuwa mwiba kwa Wafaransa hao waliotolewa kwa ulinganifu wa mabao 5-1, kwani alitia kimiani mabao yote, moja katika dakika ya 14 na jingine dakika 20 baadaye.

 

Kwa mabao hayo sasa Neymar amefikisha mabao 30 msimu huu kwa Barcelona. Licha ya kurejea baada ya kadi yake nyekundu, Zlatan Ibrahimovic hakuweza kuwasaidia Porto kukomboa mabao mawili waliyokuwa wakidaiwa.

 

Jumatano hii ni mechi ya mkondo wa pili baina ya Real Madrid wanaowakaribisha Atletico Madrid, wakiwa walienda suluhu kwenye mechi ya awali. Wakati Juventus watakuwa wageni wa Monaco. Juventus walishinda mechi ya awali kwa bao 1-0 la penati.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TETESI ZA USAJILI LEO

Stephen Keshi bosi tena Nigeria