in , ,

Barcelona watamchukua nani


*Mancini, Ferguson, Villas-Boas watajwa
*Wamo Jupp Heynckes, Enrique na Bielsa

Ulimwengu wa soka unapepesa macho kujua kocha gani atateuliwa kushika nafasi ya uongozi katika klabu ya Barcelona ya Hispania.
Mabingwa hao wamebaki bila kocha baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Tito Vilanova kuachia ngazi kwa sababu za kiafya, ambapo anasumbuliwa na saratani.
Wakuu wa Barca wanasemwa kutafuta mrithi wa Vilanova, aliyechukua nafasi hiyo baada ya kuondoka Pep Guardiola aliyemaliza likizo ya mwaka mzima na kisha kujiunga na Bayern Munich.
Wanaohusishwa na kuchukua nafasi hiyo ni pamoja na Marcelo Bielsa, raia wa Argentina ambaye hana klabu baada ya kuwa kwa misimu miwili Athletic Bilbao. Alitakiwa na klabu ya Santos ya Brazil, lakini hakupenda.
Mwingine ni Joan Francesc Ferrer ‘Rubi’ ambaye msimu uliopita alikuwa na klabu ya Girina, akakaribia kuwapandisha daraja kuingia La Liga. Amejiunga katika kikosi cha ufundi cha Barca, na alikuwa awe msaidizi wa Vilanova, hivyo huenda akafikiriwa.
Mchezaji wa zamani wa Barca, Luis Enrique naye anapewa nafasi, ambaye amepata kuwa kocha wa timu ya pili ya Barca kwa miaka mitatu, kisha akahamia Roma, kabla ya kwenda Celta msimu huu wa kiangazi.
Kocha wa Tottenham Hotspur, Andre Villas-Boas anatajwa pia katika mpango huu, ambaye amekuwa na mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London, baada ya kuwa Chelsea kwa muda mfupi.
Mwingine anayefikiriwa ni Oscar Carcia Junyen aliyekuwa mchezaji na kocha wa Barcelona, ambaye alitwaa ubingwa wa Israel wakiwafundisha Macabi Tel-Aviv. Ndiye amechukua nafasi ya Gustavo Poyet katika klabu ya nchini England ya Brighton, lakini akiitwa Barca inaelekea ataitika.
Mwingine, aliyepata kutajwa kitambo ni mchezaji wa zamani wa Barca aliyekwenda Real Madrid 1994, ambaye sasa ni kocha wa Swansea, Michael Laudrup, anayesemwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kiufundi.
Wapo wanaomfikiria Frank De Boer aliyefanikiwa katika miaka yake minne kama mchezaji wa Barcelona, tangu 1999 kabla ya kuwaongoza Ajax kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo kwenye ubingwa wa Uholanzi.
Katika hesabu hizo, yupo pia Eusebio Sacristan aliyepata pia kukipiga hapo kwenye dimba la Barca la Camp Nou. Kwa sasa ni kocha wa timu ya pili ya klabu hiyo.
Sergi Barjuan anatajwa pia, aliyekuwa klabuni hapo hapo miaka ya ’90 na alianzia kwenye timu ya vijana – La Masia.
Pengine ni wakati wa kumchukua Frank Rijkaard, Mholanzi aliyekuwa na mafanikio hapo hapo Barcelona kati ya mwaka 2003 na 2008 alipowafunda wachezaji kama Xavi, Carles Puyol na Victor Valdes ambao bado wapo. Ndiye aliwaongoza kutwaa ubingwa wa Ulaya 2006 wakiwa na wachezaji kama Ronaldinho na Samuel Eto’o. Hana klabu kwa sasa.
Zao jingine la La Masia linalotajwa kuweza kuchukua nafasi ya Vilanova ni Lluis Carreras. Pia aliyekuwa akikaimu Vilanova alipokuwa mgonjwa, Jordi Roura anatajwa kuweza kupewa nafasi hiyo.
Kocha aliyefukuzwa Manchester City, Mtaliano Roberto Mancini naye anapewa nafasi ya kuteuliwa hapo Camp Nou, na amekuwa na mafanikio ya ubingwa nchini Italia na England.
Mzee Luis Aragones (74) anahusishwa, lakini si chaguo linalotarajiwa sana, kwa sababu kwanza ameshastaafu baada ya kuwapa Hispania upingwa wa Ulaya 2008.
Huenda pia mabingwa hao wa Hispania wakafikiria kumchukua mtu ambaye Guardiola anachukua nafasi yake Bayern, Mjerumai Jupp Heynckes, aliyesema wazi kwamba ameacha kazi Bayern lakini bado hajastaafu.
Wengine wanamfikiria kocha aliyeng’atuka Manchester United, Sir Alex Ferguson, japokuwa wengi wanaona kwamba si rahisi kwake kuchukua kazi hiyo, lakini 2010 alipata kusema kwamba angependa kuwafundisha Barcelona, walau kwa mwaka mmoja.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Vilanova aachia ngazi Barcelona

*LIGI KUU YA VODACOM 2013/2014 KUANZA AGOSTI 24*