in , , ,

Barca wakaribia dili la Suarez

*Arsenal watoa dau kwa Sanchez
*Martinez, Campbell pia Emirates

Barcelona wamefanya mazungumzo yanayodaiwa kuwa mazuri na uongozi wa juu wa Liverpool juu ya kumsajili mshambuliaji wao, Luis Suarez (27).

Mazungumzo zaidi yanatarajiwa kuendelea, ambapo Barcelona wamesema wapo tayari kutoa dola milioni 127 kumpata mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Uruguay aliyefungiwa na Fifa kwa miezi minne kwa utovu wa nidhamu.

Barca walitaka kumnunua Suarez kwa bei ya chini kidogo halafu wawape Liverpool mchezaji wao mwingine raia wa Chile, Alexis Sanchez, lakini inasemekana imeshindikana kwa sababu Sanchez amesema hataki kwenda Liverpool.

Arsenal ndio wapo katika nafasi nzuri ya kumpata, kwani Sanchez (25) ameonesha kupendelea zaidi kuhamia Emirates. Anaondoka Barcelona kwa sababu hapati fursa za kutosha za kucheza mechi.

Liverpool wanadaiwa kutaka dola milioni 146, na pande zote mbili zimekubaliana kujadiliana zaidi, Liver washuke kidogo na Barca wapande kiasi ili kufikia mwafaka na kufanya mauziano ya mchezaji huyo.

Mazungumzo ya Jumatano hii jijini London yalikuwa baina ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka wa Barcelona,  Raul Sanllehi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre.

Suarez aliongeza mkataba wake na Liverpool Desemba mwaka jana, lakini kuna kifungu kinachomruhusu kuondoka iwapo klabu inayomtaka itafikia kitita kinachotakiwa, na ndicho kinachojadiliwa sasa.

Sanchez anayedhaniwa thamani yake ni dola milioni 55 amewakasirisha Barca kwa kukataa kutumiwa kama ndoano ya kumpata Suarez, akisema hataki kucheza Liverpool.

Tayari jamaa hao wa Anfield wamesajili washambuliaji Rickie Lambert na Adam Lalana, na wanadhaniwa kwamba wataongeza mwingine ili kupata mafanikio kama ya msimu uliopita ambapo Suarez alishirikiana vyema na Daniel Sturridge.

Kocha Arsene Wenger wa Arsenal anadaiwa kuweka mezani kwa Barcelona ofa ya pauni milioni 32 kwa ajili ya kumnasa Sanchez anayetakiwa pia na Juventus na Manchester United. Wenger atakutana na wakala wa Sanchez nchini Brazil wiki hii kuweka mambo sawa.

Barcelona wamesema wazi mapema kwamba wapo tayari kumwachia Sanchez aende timu anayotaka. Arsenal wanahitaji kuongeza nguvu kwenye ushambuliaji ambako kunapwaya na mpachika mabao pekee anayetegemewa ni Olivier Giroud.

Arsenal wameripotiwa kumsajili beki wa kulia wa Newcastle, Mathieu Debuchy kwa pauni milioni 12 lakini taarifa zake rasmi zitatolewa baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil .

Debuchy (28) anakwenda kuchukua nafasi ya Bacary Sagna aliyehamia Manchester City baada ya mkataba wake Arsenal kumalizika. Debuchy ndiye yupo katika kikosi cha kwanza cha Ufaransa kwenye Kombe la Dunia, Sagna akiwa papili wake.

Mfaransa huyo kama alivyo Sagna, aliwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita kwamba alikuwa na hamu sana ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, na alikuwa akitafutwa pia na Paris Saint-Germain na Real Madrid.

Kadhalika Arsenal wanamrejesha mchezaji wao aliyekuwa Olympiakos kwa mkopo, Joel Campbell ambaye ametamba sana kwenye fainali za Kombe la Dunia akichezea Costa Rica.

Campbell (22) ni mshambuliaji wa kati na ameshaambiwa kwamba aripoti klabuni baada ya likizo yake tayari kuanza ziara ya kabla ya msimu na wachezaji wenzake. Atakuwa akichuana kupata namba na Giroud, Lukas Podolski na Yaya Sanogo.

Washika Bunduki wa London pia wamemsajili kiungo wa West Ham United, Ben Sheaf anayechezea pia Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 ya England. Sheaf (16) amehamia Emirates baada ya kukataa mkataba mpya na Hammers.
Sheaf anachukuliwa kuwa mmoja wa viungo mahiri zaidi vijana nchini England.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa Porto na Colombia, Jackson Martinez amesema anapenda kujiunga na Arsenal, timu aliyoishabikia tangu akiwa mtoto. Martinez (27) amesaidia Colombia kufika robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu.

 Amefunga mabao 60 katika mechi 90 na inaelezwa kwamba Wenger yupo tayari kutoa pauni milioni 35 ili kufikia kigezo cha kuondoka kwake kilichowekwa kwenye mkataba wake na Porto.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wambura, wengine wasimamishwa uanachama Simba..

Wajerumani wapata homa