in , , ,

Bacary Sagna asajiliwa Man City

Hatimaye beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna amekamilisha usajili wake Manchester City kwa kupewa mkataba wa miaka mitatu.

Sagna amemaliza mkataba wake Arsenal, ambapo wakuu wa Emirates walikuwa wakivuta miguu kumpatia mkataba mpya kwa sababu ya umri wake.

Sagna (31) alikuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio Arsenal msimu uliomalizika majuzi lakini Arsenal waliona kwamba umri na fedha alizokuwa akidai vilikuwa juu.

Inaelezwa kwamba awali alipewa mkataba wa mwaka mmoja Arsenal akakataa, akapewa wa miaka miwili lakini wakashindwana kwenye malipo, akaamua kuondoka.

Alicheza mechi yake ya mwisho kwenye fainali ya Kombe la Ligi wikiendi iliyopita ambapo Arsenal waliibuka na taji baada ya miaka tisa.
Inaelezwa kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamempa mkataba ambao atalipwa pauni 150,000 kwa wiki, ikiwa ni nyongeza kubwa kutoka pauni 80,000 alizokuwa akilipwa Arsenal.

Hata hivyo, Sagna ambaye kocha Arsene Wenger alijaribu kumbakiza, alikuwa akitaka nyongeza hadi pauni 200,000 na miaka mitatu zaidi hapo Emirates, kiwango ambacho kikilinganishwa na umri wake waliona hakikidhi mahitaji.

Sagna alikuwa pia akitakiwa kusajiliwa na klabu nyingine kubwa Ulaya kama Paris Saint Germain,  na Monaco za Ufaransa na  Galatasaray ya Uturuki.

Kutokana na mazingira hayo, Arsenal wameshaanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili Serge Aurier anayecheza Toulouse ya Ufaransa kuziba nafasi ya Sagna.

Aurier anayethaminishwa kwa pauni milioni saba amesema wazi kwamba hawezi kukataa ofa kutoka klabu yoyote ya Ligi Kuu England, hata zilizopanda daraja msimu huu kwa sababu ni ligi kubwa.

Arsenal wameshaanza mazungumzo na klabu yake, ambapo watalazimika kutoa fungu huku Sagna, akiondoka na kusajiliwa bure huko aendako kwa kuwa ni mchezaji huru.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Moyes azua kizaazaa baa

Usajili Man United bado