Baada ya Arsenal kumsajili Petr Cech, je nani afuate?

Haya ni maoni yangu juu ya usajili wa Arsenal, nani wamuongeze, na kwanini Wenger alimkomalia sana huyu golikipa….nionavyo mimi, mzee Wenger, amekitumia vizuri kipengele cha wachezaji wa nyumbani na wa nje, hivyo kupata nafasi moja zaidi, kwa kumtoa Ospina, na Cech kuingia kama mchezaji wa nyumbani…hivyo….Kufanikiwa kwa Arsenal kumsajili Cech na labda wakimwachia Ospina kutawapa nafasi ya kusajili mchezaji anayejitajika sana katika nafasi ya kiungo cha ukabaji au mlinzi.

Haikumithilika kwa muda mrefu kwa wengi Chelsea kujiunga Arsenal, lakini Wenger alikuwa na wazo naye kwa muda mrefu, na msimu wa 2013/14 alidhani angeweza kumpata ikiwa Courtois angekuwa Stamford Bridge.

Comments