in , , , ,

ASHANTI UTD, SIMBA UWANJANI VPL

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
zinaanza kesho (Novemba 6 mwaka huu) ambapo Ashanti United itakuwa mwenyeji
wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya
mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na
sh. 20,000. Waamuzi wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote
kutoka Pwani wakati mezani atakuwa Hamisi Chang’walu.

Mechi nyingine za kesho ni JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa
Chamazi), Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na
Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Keshokutwa (Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza
itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa
kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja
wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino
Rangers na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro
JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons.

*TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA*

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya
mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha
orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.

Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya
uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote
waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa
au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.

Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao
(vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote
waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).

*TANZANITE KWENDA MAPUTO KESHO*

Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa
kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla ya kuanza safari ya kwenda
Maputo, Msumbiji.

Hafla fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi
kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa
ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.

Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu
wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa
Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana kwa
ndege ya LAM.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Malinzi kuhamisha makao ya TFF..

Man City wawapiga CSKA Moscow