in , , ,

Arsene Wenger atimiza miaka 20 Arsenal

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 20 tangu ajiunge na
klabu hii ya London Kaskazini.

Amefanya mengi hapo na anaaminiwa sana na wamiliki japokuwa kuna
washabiki wanamtilia shaka juu ya baadhi ya uamuzi anaochukua, hasa
kujivuta sana katika kusajili wachezaji wenye majina makubwa.

Aliingia akiwa kijana, akaleta mapinduzi yake na kuingiza falsafa
tofauti na sasa ndiye kocha mkongwe zaidi katika Ligi Kuu ya England
(EPL). Alhamisi hii ni siku ya Wenger, ametimiza miaka 20 tangu aingie
hapa akitoka Japan.

Mfaransa huyu mrefu na mwembamba alivuta hisia za wengi alipowasili,
baadhi wakiwa na shaka iwapo angeiweza kazi, ikizingatiwa kwamba
alikuwa ametoka Japan ambako soka haikuwa maarufu.

Ni yeye aliyewezesha ujenzi wa uwanja mkubwa wa kisasa wa Emirates, wa
pili kwa ukubwa miongoni mwa klabu baada ya ule wa Old Trafford wa
Manchester United. Aliwezeshaje? Kwa kuchagua kujengwa uwanja badala
ya kununua wachezaji.

Pengine hiyo ni moja ya sababu za mtaalamu huyu wa uchumi kwa kusomea
amekuja kuitwa profesa. Amewezesha wamiliki kujichumia kiasi kikubwa
cha fedha na kwa hilo wanafurahia huku washabiki wakisonya kwa
kutotwaa ubingwa.

Hata hivyo, mmoja wa wamiliki, Stan Kroenke, bilionea wa Marekani
anasema wazi kwamba hakununua klabu hiyo ili watwae ubingwa,
akionekana kupishana kabisa na washabiki na kumsababisha Wenger
kutabasamu.

Kwa miaka mingi sasa Arsenal wamekuwa wakionekana kulinyemelea taji la
ubingwa lakini matumaini hupukutika kwa kuishia ama nafasi ya pili,
tatu au ya nne. Kubwa ambalo wamekuwa wakijihakikishia ni kucheza Ligi
ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Feguson na Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Sam Allardyce wamekiri
kwamba wanawiwa na Wenger na wanamchukulia kuwa mmoja wa makocha bora
duniani. Mambo yangeweza kuwa tofauti, kwani awali Arsenal walikuwa
wakifikiria kumchukua Bobby Robson kuwa kocha wao wa muda mrefu.

Robson, inaelezwa, alishakubali kabisa kujiunga lakini akashawishiwa
na Porto kubaki kwenye klabu hiyo kubwaya Ureno. Wenger mwenyewe
alikuwa amewekwa kwenye orodha lakini akionekana kuwa mbadala ghali
zaidi.

Alikutana kwanza na David Dein chakulani aliyekuwa naibu makamu wa
Arsenal mnamo 1989 . wakazungumza na Dein alivutiwa naye kutokana na
uchangamfu wake lakini pia alivyokuwa akisakata dansi.

Miaka saba baadaye alitambulishwa Highbury, uwanja waliokuwa wakitumia
Arsenal. Ilikuwa Jumapili ya Septemba ambapo watu wakashangaa kufanana
kwa majina, yaani Arsenal na Arsene.

Wenger aliingia muda mwafaka Arsenal, kwani wahusika walikuwa tayari
kwa mapinduzi, na aliyaanzisha na kufanikiwa, wakaanza soka ya kupena
pasi fupi fupi na kumiliki mpira zaidi huku ufungaji mabao ukiwa ni
‘yatokanayo’ tu.

Ni huyu ambaye katika kipindi cha miaka 12 iliyofuata, vyombo vya
habari vya England vilikuja kumtaja mara 703 kuwa ni ‘profesa’. Miaka
20 baadaye yupo pale pale akiendelea na kazi yake bila wasiwasi.

Ameweka rekodi kwenye soka ya England, kwani ndiye kocha wa kwanza
kutoka ng’ambo kufanikiwa, wa kwanza kuchagiza utamaduni wa Kiingereza
na amekuwa akitaka kuwekwa sheria na kanuni kali juu ya usajili,
akilia na jinsi wachezaji wanavyopandishwa bei isivyo sawa.

Ni Wenger aliyembadilisha Thierry Henry kutoka kuwa winga hadi kuwa
mpachika mabao hodari aliyekuwa juu sana hadi kuondoka kwake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man United hoi Europa

Tanzania Sports

Ushindani mkubwa EPL