in , , ,

ARSENAL YAZAMISHWA UGENINI (CL)

Michezo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea hapo jana Jumatano ambapo timu 16 kutoka kwenye makundi manne zilionyeshana kazi kwenye viwanja tofauti. Jumla ya mabao yaliyofungwa yalikuwa 28. Haya hapa ni matokeo ya michezo hiyo.

CHELSEA YATAKATA

FAV
Chelsea wakiwa nyumbani waliwaadhibu Maccabi Tel-Aviv kutoka Israel

Chelsea wakiwa nyumbani waliwaadhibu Maccabi Tel-Aviv kutoka Israel kwa mabao manne kwa sifuri kwenye mchezo wa Kundi G. Mapema kwenye dakika ya 6 ya mchezo huo Eden Hazard alikosa penati ambapo alipiga shuti lililopaa mno juu ya lango. Baadae Willian alifungua kitabu cha mabao kisha Oscar, Diego Costa na Cesc Fabregas wakakamilisha hesabu.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hili Dynamo Kyiv ya Ukraine ilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na FC Porto ya Ureno. Walikuwa Oleg Gusev na Vitaly Buyalsky waliofunga mabao ya Dinamo Kyiv huku Vincent Aboubakar akiifungia FC Porto mabao yote mawili,

ARSENAL YAZAMISHWA UGENINI

Washika Bunduki wa London kwenye mchezo wa Kundi F wakiwa pungufu baada ya Olivier Giroud kuonyeshwa kadi mbili za manjano walilazimika kuchezea kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Dinamo Zagreb ya Croatia kwenye dimba la Stadion Maksimir.

Zagreb walipata bao la kuongoza kwenye dakika ya 24 kupitia kwa Josip Pivaric na baadae Junior Fernandes akaongeza bao la pili kwenye dakika ya 58. Bao la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Theo Walcott kwenye dakika ya 79 akimalizia kazi nzuri ya Alexis Sanchez.

Bayern Munich wakiwa ugenini walijiweka kileleni mwa kundi hili baada ya kuwafunga Olympiacos mabao matatu kwa sifuri. Thomas Muller alifunga mawili na Mario Gotze alifunga moja akitokea benchi.

BARCELONA YASHIKILIWA NA ROMA

Barcelona walishindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare
Barcelona walishindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare

Kwenye Kundi E mabingwa watetezi FC Barcelona walishindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya AS Roma kwenye dimba la Stadio Olympico jijini Rome hapo jana.

Mabingwa hao walitangulia kupata bao kwenye dakika ya 21 kupitia kwa Luis Suarez aliyefunga kwa kichwa akipokea krosi ya Ivan Rakitic. Dakika 10 baadae likafuata bao la ajabu alilofunga Alessandro Florenzi kutokea umbali wa mita 56, bao ambalo likaipatia Roma sare.

Bayer Leverkusen walipata matokeo ya mabao manne kwa moja dhidi ya Bate Borisov ya Belarus na kushika nafasi ya juu kwenye kundi hili ambapo Barcelona na Roma zinafuata kwenye nafasi ya pili na Bate wanashika mkia.

Kwenye michezo mingine Valencia ya Kundi H ikicheza nyumbani imekuwa timu pekee kutoka Ligi Kuu ya Hispania kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye michuano hii baada ya kukubali kipigo cha mabao matatu kwa mawili dhidi ya Zenit St. Petersburg ya Urusi.

Hulk alitangulia kuipatia mabao mawili Zenit kabla ya Valencia kusawazisha kupitia kwa Joao Cancelo na Andre Gomes. Zenit wakapata bao la ushindi kupitia kwa kiungo Mbelgiji Alex Witsel robo saa kabla ya mchezo kumalizika.

Mchezo mwingine wa kundi hili ulikuwa baina ya Gent ya Ubelgiji na Olympic Lyon ya Ufaransa ambazo zilifungana bao moja kwa moja. Lyon walipata nafasi ya kupata bao la ushindi mwamuzi alipowazawadia penati dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika lakini mshambuliaji Alexandre Lacazette aliichezea nafasi hiyo

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NI WAKATI WA SAMATA NA ULIMWENGU

Tanzania Sports

Rais Jakaya Kikwete afungua majengo pacha ya PSPF