in , , ,

ARSENAL v. TOTTENHAM

 

 

Baada ya kushinda michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu ya England, Arsenal walio kwenye nafasi ya pili wakiwa na jumla ya alama 25 hapo kesho watawakaribisha Tottenham Hotspur kwenye dimba la Emirates kwenye mchezo wa mzunguko wa 12 wa ligi hiyo.

Washika bunduki hao wa London ambao Jumatano walipokea kipigo cha 5-1 kutoka kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wanahitaji alama tatu kwenye mchezo huo wa hapo kesho kwa ajili ya kuendeleza mbio zao za ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.

Tottenham wanaonolewa na Mauricio Pochettino bado hawajapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu ya England tangu walipofungwa 1-0 na Manchester United kwenye mchezo wa ufunguzi uliopigwa Agosti 8. Kwa sasa wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na alama 20.

Rekodi za michezo ya karibuni baina ya timu hizi zinaonyesha kuwa Tottenham wameshinda mchezo mmoja tu kati ya michezo 22 iliyopita waliyopiga ugenini dhidi ya Arsenal.

Kwenye msimu huu timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa Kombe la Ligi mwezi Septemba ambapo Arsenal walishinda mchezo huo uliopigwa ndani ya dimba la White Hart Lane kwa mabao mawili kwa moja.

Takwimu za EPL msimu huu zinaonyesha kuwa Arsenal wamefunga jumla ya mabao 21 mbaka sasa huku Tottenham wakiwa wamefunga mabao 19. Kwa upande wa mabao ya kufungwa, Arsenal wamefungwa mabao 8 wakati Spurs wamefungwa mabao 9.

Pia takwimu za wastani wa idadi ya mashuti kwa mchezo mmoja Arsenal bado wako mbele. Wao ndiyo timu yenye wastani wa mashuti mengi zaidi kwa mchezo mmoja wakiwa na wastani wa mashuti 19 kwa mchezo. Tottenham wao wana wastani wa mashuti 16 kwa mchezo mmoja wakiwa kwenye nafasi ya tatu.

Advertisement
Advertisement

Takwimu za umiliki wa mpira zinaonyesha kuwa Arsenal na Tottenham zote zipo kwenye timu tano za juu zenye wastani mkubwa wa umiliki mpira. Arsenal wapo kweye nafasi ya tatu wakiwa na asilimia 57 na Spurs wapo kwenye nafasi ya tano wakiwa na asilimia 54.

Takwimu hizo za wastani wa idadi ya mashuti kwa mchezo mmoja na za wastani wa umiliki wa mpira zinaonyesha kuwa timu zote hizi zinacheza mpira wa kushambulia zaidi. Hivyo tutarajie soka la kuvutia kwenye mchezo wa kesho unaofahamika kama ‘North London Derby’.

Kwa upande wa vikosi wenyeji Arsenal bado wanaendelea kuandamwa na wimbi la majeruhi kwenye kikosi chao. Majeruhi Theo Walcott, Aaron Ramsey na Hector Bellerin watakuwa nje. Kuna mashaka kuwa Laurent Koscielny pia anaweza kuwa nje kutokana na majeraha.

Majeruhi wengine wa Arsenal ni Oxlade-Chamberlain, Jack Wilshere, Danny Welbeck na Thomas Rosicky. Tottenham wao wanao majeruhi wawili pekee ambao ni Alex Pritchard na Nacer Chadli.

Nyota wa kutazamwa kwa upande wa Arsenal ni Olivier Giroud na Mesut Ozil. Giroud amefunga mabao matano kwenye michezo saba iliyopita ya EPL. Kiungo Mjerumani Mesut Ozil ndiye anayeongoza kwa pasi za mabao kwenye ligi tano kubwa za Ulaya akiwa na pasi 9 za mabao.

Kwa upande wa Tottenham nyota wa kutazamwa hapo kesho ni Harry Kane. Mshambuliaji huyu kijana aliuanza msimu huu vibaya lakini kwa sasa ameshafunga mabao matano yakiwemo manne aliyofunga kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya AFC Bournemouth na Aston Villa.

 

Mechi nyingine za EPL
Mechi nyingine za EPL

 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HAYA NDIYO MATATIZO YA CHELSEA

Tanzania Sports

Chelsea ni kupigwa tu