in , , , ,

Arsenal, Besiktas ngoma mbichi

Arsenal wamekwenda suluhu na Besiktas katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) jijini Istanbul, Uturuki.

Vijana hao wa Arsene Wenger walimaliza mchezo na watu 10 baada ya Aaron Ramsey kutolewa nje kwa kupata kadi mbili za njano, na sasa hatima ya nani ataingia hatua inayofuata itaamuliwa Emirates Jumatano ijayo kwenye marudio.

Kwa ujumla timu zilitoshana nguvu, kila moja ikikosa nafasi kadhaa, ikiwa ni pamoja na mkwaju wa Demba Ba wa Besiktas kugonga mwamba dakika za mwanzo huku ule wa Alex Oxlade-Chamberlain wa dakika za mwisho nao ukipigishwa kwenye mlingoti wa goli na kipa Tolga Zengin.

Arsenal wanasaka nafasi hiyo kwa msimu wa 17 mfululizo na Wenger amesema wataitafuta kwa gharama yoyote ile, akisema kucheza UCL si kwa ajili ya fedha bali heshima kubwa ya klabu barani Ulaya na duniani kwa ujumla.

Ba alijiunga Besiktas baada ya kutopewa muda wa kutosha kucheza Chelsea, na sasa amemkandia kocha Jose Mourinho kwamba hakuwa akimpanga kwa vile amezoea kupanga wachezaji kwa majina yao na unyota wao bila kuangalia viwango. Alikuwa nusura ajiunge Arsenal msimu uliopita.

Baada ya Ramsey kutolewa nje dakika ya 79, ilidhaniwa Besiktas wangetumia mwanya huo kuibuka na ushindi, lakini ndio kwanza Arsenal wakaonekana kuwa wazuri isipokuwa muda ukawatupa mkono.

Olivier Giroud aliyecheza kama mshambuliaji wa kati hakuwa kwenye kiwango kizuri na mashabiki wa Arsenal wanaona kuna haja ya kusajili mchezaji wa kiwango kikubwa zaidi kwenye eneo hilo, ikiwa wanataka kuzoa mataji msimu huu. Yaya Sanogo aliachwa London kwa sababu za kiafya.

Ramsey alitolewa nje kwa kosa la kuvuta jezi ya kiungo Oguzhan Ozyakup akiwa karibu nusu ya uwanja, na aliivuta kwa nyuma baada ya kupoteza umiliki wa mpira, ambapo Wenger analalamikia kadi zote mbili, akidai kuna rafu nyingine nyingi zaidi zilifanyika, lakini wao ndio wanarudi London Ramsey akikosa mechi ijayo.

Ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa Wales kupewa kadi nyekundu kwenye mashindano makubwa akiwa na klabu yake hiyo.

Kocha wa Besiktas aliyepata kucheza Everton na West Ham za England, Slaven Bilic naye alitolewa nje na atakosa mechi ijayo kwa kosa la kulalamika kupita kiasi dhidi ya waamuzi kwa mambo yasiyokuwa na msingi.

Nahodha wa Arsenal, Mikel Arteta aliumia dakika ya 48 na kutolewa nje. Wenger hakutumia wachezaji wake wa Ujerumani, Per Mertesacker, Lukas Podolski wala Mesut Ozil wanaoendelea na mapumziko, wakitarajia kuanza kucheza Jumamosi ijayo dhidi ya Everton.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Fifa wamrejesha kitini Maigari

Dunga aisuka upya Brazil