in , ,

Anna Bayi kutogombea tena Chaneta..

Mama Anna Bayi kushoto

*Ni uamuzi mzuri

 

Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Bayi ametangaza rasmi kuwa hatagombea tena ili kutetea nafasi yake wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Machi 23 mjini Dodoma.

Akizungumza jijini  jana, Bayi alisema kuwa ameamua kuachia kung’atuka ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine wenye sifa kujitokeza na kuongoza chama hicho kwa matarajio ya kuleta mawazo mapya na kuendeleza mchezo huo nchini.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa muda aliotumia kukaa madarakani unatosha kwake na kwamba, anaamini kuwa akishirikiana na wenzake, amesaidia kuipa Chaneta mafanikio makubwa, yakiwamo ya kuipeleka timu ya taifa kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa.
“Nimeamua kutogombea tena ili kutoa nafasi kwa wadau wengine kuendeleza gurudumu la netiboli nchini,” alisema Bayi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi, aliwasihi watu wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania uongozi katika chama chao.
Akizungumza jana, Mkisi alisema kuwa tangu watangaze tarehe ya kutoa fomu hizo, hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza kuchukua fomu hadi sasa, isipokuwa
wamepokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa baadhi ya wanamichezo kutoka mikoani kuwa wanahitaji fomu za kuwania ujumbe.
“Tunaomba wanamichezo wenye sifa wachangamkie fursa hii ya kuchukua fomu za kuwania uongozi,” alisema Mkisi, akiongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu hizo ni Machi 15 na usaili utafanyika Dodoma Machi 21.
Nafasi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na za mwenyekiti, katibu mkuu, mweka hazina na wajumbe.
Katika hatua nyingine, Chaneta imetaka mikoa kulipa ada ya uanachama kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu kufika.
Mkisi alisema mikoa itakayoshindwa kulipia ada ya uanachama haitaruhusiwa kutoa wawakilishi wa kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.
Awali, uchaguzi wa Chaneta ulikuwa ukipigwa kalenda mara kadhaa kutokana na baadhi ya mikoa kusuasua kuitisha chaguzi zake na pia, baadhi yao kushindwa kulipia ada za uanachama.
Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea wapoteza nafasi ya tatu

Kenyans sweep gold at beach Volleyball tour in Burundi