in

Ali Kiba, Samatta, uso kwa uso Taifa

Lengo likiwa lilelile kuwavutia watu kufika uwanjani

Msanii wa Bongo Flava Ali Kiba kuungana na nyota wa Aston Villa  ya England, Mbwana Samatta kukutana uwanja wa taifa kwa ajiri ya tamasha lao ‘Nifuate’.

Tamasha hilo litakuwa la mchezo wa mpira wa miguu kama walivyowahi kufanya huko nyuma ikiwa na lengo la kuchangisha ili wasaidie watu wenye uhitaji maalumu.

Hii sio mara ya kwanza itakuwa safari ya tatu yote ikifanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mwaka huu litafanyika Augusti 2 katika uwanja huo na mwaka huu itakuwa wameahidi kulifanya bora zaidi.

Kwa mujibu wa wa Kalenda Agusti 2 itakuwa siku ya jumamosi, mwaka huu wameongeza kitu kwani kabla ya mchezo kutakuwa na burudani mbalimbali.

Tayari msanii Ali Kiba kutoka Kings Music K2ga atalipamba tamasha hilo.

Kama ulikuwa hujui lengo kuu la tamasha hili ni kuchangisha fedha na kuzitoa sehemu zenye uhitaji.

Yaani Kiba na Samatta wameangalia watatumiaje umaarufu wao na kujaza watu uwanjani kwa faida ya wale wenye uhitaji.

Katika uchaguzi wao wa wachezaji huwa wanawachukua wale wanaocheza ligi kuu pamoja na wasanii wa muziki, wanaungana na kufanya tamasha lionekane bora kabisa.

Lakini pia kwa upande wa makocha wanachukua waliokuwa na CV nzuri kabisa mfano msimu wa kwanza walimchukua  Jamhuri Kihwelo huku Maafisa habari wakiwa kina Joti, Haji Manara na Mpoki .

Lengo likiwa lilelile kuwavutia watu kufika uwanjani ili wapate wanachokihitaji.

Yaani huwa wanajitolea kwa nguvu zao zote na uzuri wake hawakati tamaa, na ndivyo Watanzania tulivyo.

Ili kuonesha utofauti wa msimu mingine iliyopita mwaka huu washazitangaza jezi zitakazo tumika muda mrefu kabla ya mchezo.

Agusti 2 Samatta atakuwa amerudi likizo kwa ajiri ya msimu ujao hatujui kama timu yake itabaki ligi kuu au itashuka daraja ila tunaomba dua isishuke.

Kitu chakuvutia 

Samatta amecheza ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza na ametengeneza historia ya aina yake msimu huu kwani amefunga katika uwanja wa Wembly kwa mara ya kwanza, anaungana na Didier Drogba na Waafrika wengine kuwahi kufunga katika fainali ya kombe la ligi maarufu kama ‘EFL’ zamani Carling Cup.

Watu wanataka kumuona Samatta japo dakika 10 akionesha vitu vyake uwanjani baada ya kuwa staa wa EPL.

Ali Kiba naye amebakia kuwa mwanamuziki mwenye heshima kubwa Tanzania kwa upande wa Bongo Flava, amekuwa akitoa vibao vizuri, mara tu anapotoa na vimekuwa vikikubaliwa na shabiki zake.

Sasa anatamba na ngoma inayoitwa ‘So hot’ wengi wakisema kuwa amebadilika kwa muziki aliokuawa anaimba hapo awali.

Macho na masikio yapo kwa Samatta na Kiba wachezaji gani watawachagua msimu huu?

Ifikapo Julai 25 watakuwa washaanza kutaja majina yao na kujua mchezaji gani atakuwa timu ipi.

Samatta amekuwa mshindi wa mara zote alipo anza kufanya tamasha lao .

Ukitaka kugundua kuwa mchezo wa mpira wa miguu una raha yake na una thamani kubwa duniani angalia endapo kuna hamasa yoyote ya kuchangia kitu utawaona watu mbalimbali wakijumuika.

Kama wasanii wa kuimba watajumuika na kuunda timu yao, kuwaburudisha mashabiki wao ambao watakuwa uwanjani kwa ajiri ya shughuli hiyo.

Ndio maana tumeshawahi kuona matamasha makubwa yakihusu mpira wa miguu, hapa Tanzania huwa yanafana sana.

ANGALIZO : Ali Kiba na Mbwana Samatta wanatakiwa wafanye tathimini sasa baada ya msimu huu wa tatu kweli wanapata wanachokitarajia? kama hawapati wakae chini wabuni njia nyingine ya kuongeza utamu zaidi.

Ni wazo zuri sana na huwa lina maana kubwa sana kwa wahitaji kupitia umaarufu wao wanatengeza faraja kwa wengine.

Wazo la Mwandishi

Ali Kiba na Samatta ni ‘Brand’ zinazojitegemea nafikiri hawashindwi kutafuta wadhamini wakulisimamia tamasha lao.

Kama walivyokaaa na kuwawazia mashabiki zao sasa waongeze ubunifu wawafuate wadhamini waingie  nao mkataba ili hata mashabiki wakiingia wachache iwe sababu ya kupata kipato upande wa pili na hii itasaidia kuona faida ya kuungana kwao.

Lakini pia wafanye wiki nzima au zaidi ya ‘Promotion’  ikifikia kukaribia kilele cha tamasha lenyewe.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Manara, Muro, Nugaz nani zaidi?

Manara, Muro na Nugaz nani zaidi?

Aishi Manula

Mikono ya Manula imempoteza Kakolanya?