in , ,

Manchester City: waleteni hao Inter Milan sasa

ILIWACHUKUA sekunde 13 tu mabingwa wa EPL, Manchester City kupachika bao la kuongoza katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya majirani zao Manchester United. Bao hilo lilifungwa na kiungo na nahodha wao Ilkay Gundogun katika dimba la Wembley. Bao la kwanza la Man City limeandika historia kufungwa mapema zaidi katika mchezo wa fainali. 

Katika mchezo huo uliojaa ufundi na msisimko mkubwa TANZANIASPORTS imefuatilia rekodi na habari za kusisimua katika fainali ya FA msimu huu na hapa inakuletea tathmini juu ya kile kilichutokea katika mchezo huo wa maimba miwili ya jiji la Manchester.

Wakati Man City wakinyakua taji hilo la pili, sasa macho na masikio ya wengi yatakuwa kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambako watakutana na miamba ya Italia, Inter Milan. Ubingwa waliochukua Man City ni kama vile wametuma ujumbe kuwa ‘waleteni hao Inter Milan’. Na bila shaka Inter Milan na benchi la ufundi lote pamoja na viongozi wametzama mechi za Man City na kujipanga namna ya kukabiliana na ‘dude’ hilo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Bao la mapema

Bao la kwanza la Manchester City lililofungwa na nahodha wao Ilkay Gundogun lilikuwa la mapema zaidi. Gundogan alifunga bao hilo katika sekunde ya 13 tangu kuanza mchezo huo.  Bao hilo limefikia rekodi iliyoandikwa na mshambuliaji wa zamani wa Everton, Louis Saha katika mchezo dhidi ya Chelsea mwaka 2009 kwenye fainali ya Kombe la FA.

Tanzania Sports

‘Kikongwe wa mabao’

Mabao mawili aliyofunga katika mchezo wa fainali ya FA yanaweza kutajwa ni kuwa ni mchezaji kikongwe ambaye amebakiwa na makali yake. Kibarua kigumu ni namna ambavyo uongozi wa Man City utakubali kuwa nyota wao Ilkay Gundogan aondoke klabuni kwa kigezo cha umri kumtupa mkono. Ni nahodha wao kwa sasa, na ameonesha umahiri mkubwa msimu huu wakati akelekea ukingoni mwa mkataba wake. Gundogan ni kikongwe ambacho kimeipa ushindi Man City hali ambayo nyota mwenzake Jack Grealish akiri kuwa ndiye mwokozi wao kwa sasa. 

Bao la Kapteni wa Man United

Nahodha wa mchezo wa fainali wa klabu ya Manchester United, Bruno Fernandes amekuwa wa kwanza kufunga bao katika mchezo w afainali ya FA. Alikuwa Eric Cantona ambaye aliandika rekodi kwa kufunga bao katika mchezo wa fainali ya FA mwaka 1996. Hivyo Bruno anakuwa nahodha wa pili.

Nani kuzuia Man City?

Inavyoonekana hadi sasa timu zimekosa maarifa ya kuizuia Man City katika soka. Ni timu nzuri ambayo imejipanga kufanya vizuri. Msimu huu wamefanikiwa kujilinda vizuri kuliko misimu iliyopita. Hata hivyo wasiwasi pekee uliopo sasa, ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa dhidi ya timu hiyo kuhusu ukiukwaji wa sharia za usajili. Ikiwa Man City hawatakutwa na makosa maana yake inakuwa si timu tena ni kama vile ni dude la kutisha linalotamba viwanjani.

Man Cify kusaka rekodi ya Man United

Mwaka 1999 Manchester United ikiongozwa na gwiji la ukocha duniani, Sir Alex Ferguson ilitwaa makombe matatu msimu huo na kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka jiji la Manchester. Hakuna timu nyingine kutoka jiji la Manchester iliyowahi kutwaa mataji matatu katika msimu mmoja. Ferguson alikuwa kwenye kilele cha mafanikio ambacho sasa Man City nao wanakitafuta. Man City wanataka kufikia rekodi hiyo, ambapo sasa wametwaa mataji mawili ya EPL na FA huku wakielekea kwenye mchezo mwingine wa fainali ya Ligi ya Mabingwa. Je watafikia rekodi ya Man United? Tusubiri. 

Pep Guardiola amejaza lita ya timu yake

Katika kikosi cha Man City wachezaji wanachezeshwa kwa mzunguko. Katika kikosi kilichoanza dhidi ya Man United, golikipa alikuwa Moreno akichukua nafasi ya Edersson. Katika kikosi hicho wachezaji wazuri kama kama Phil Foden, Aymeric Laporte, Nathan Ake wanakuwa benchi ikiwa na udhihirisho kuwa timu hiyo inao wachezaji wengi wenye viwango vya juu. 

Ni timu yenye kikosi kipana au sawa na kusema ujazo wa lita yao umefika pazuri zaidi. Anayeingia ni sawa na anayetoka, ni kama vile kuna nafuu na afadhali ambazo zote zinakuwa na mchango mmoja. Guardiola ameunda timu kali na yenye ushindani kila idara hali ambayo inawapa wakati mgumu wapinzani wao. 

Ten Hag ameleta zama mpya

Ni kama vile Man United inaamka usingizini. Ni timu ambayo imepitia nyakati za giza tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson katika kiti cha ukocha wa timu hiyo. Wamepta makocha wengi kama David Moyes, Jose Mourinho, Louis van Gaal, Ryan Giggs lakini haikuwahi kuchanua kwa mafanikio. Msimu huu Man United wamecheza fainali mbili za mashindano. 

Fainali ya kombe la Carabao ambalo wamelitwaa na fainali ya FA ambayo wamefungwa na Man City. Ikumbukwe huu ni msimu wake wa kwanza tangu achukue jukumu la kuinoa Man United akitokea Ajax Amsterdam. Lililo bora zaidi Man United wamefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Ni dhahiri kocha wao mholanzi Eric Ten Hag ameleta zama mpya Old Traford. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ni ufalme wa Man City au Man United?

Tanzania Sports

Machozi ya Nabi ni mzigo mpya wa klabu za Tanzania