in , ,

30 TWIGA STARS WAITWA KAMBINI

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa
kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.

Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka
huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya
wachezaji kurudi kwenye klabu zao.

Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na
kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi
ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.

Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati
Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester
Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn
Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).

Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda
(Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna
Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati
Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).

Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord
Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida
Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC
Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

*RCL KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO*

Raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26
mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita
tofauti.

Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro
itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini
Moshi.

Nayo Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya
Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda
mkoani Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC
na Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya
Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Leo (Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza
na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za
marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya
Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na
16 mwaka huu.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

BMT ifanye haya kukuza michezo Nchini

Bayern Munich mabingwa Ulaya