Ni Ronaldo tena

Nyota wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa
mwanasoka bora wa mwaka na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Ronaldo amemshinda hasimu wake, Lionel Messi wa Barcelona na Argentina
kwenye kinyang’anyiro hich0, na alitajwa kwenye hafla iliyofanyika
Zurich, Uswisi, kunako makao makuu ya Fifa.

Ronaldo (31) licha ya kumbwaga Messi, alikuwa pia mbele ya Antoine
Griezmann wa Atletico Madrid, ajabu ni kwamba watatu bora hao wote
wakitoka klabu za Hispania.

Ronaldo alitangazwa kuwa mshindi na kukabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or
Desemba mwaka jana, baada ya kuwa na msimu wenye mafanikio, ambapo
Real Madrid walitwaa ubingwa wa Ulaya.

Carli Lloyd wa Marekani alitajwa kuwa mwanasoka bora zaidi wa kike
huku Kocha wa Leicester, Claudio Ranieri akitajwa kuwa kocha bora wa
mwaka 2016.

Kura hupigwa na manahodha wa timu za taifa pamoja na makocha, lakini
pia baadhi ya waandishi wanaochaguliwa na kwa mara ya kwanza safari
hii kulikuwapo kura mtandaoni kutoka kwa washabiki.

Ronaldo alijiunga na Real Madrid 2009 akitoka Manchester United;
amekuwa mtamu kwenye kufunga mabao, na kwa kiasi kikubwa yake imekuwa
‘the one man show’. Akipenda zaidi mafanikio yake kuliko klabu.

Amekuwa akitaka afunge zaidi yeye kuliko kuachia wenzake. Akishindwa
kufunga hukasrika na wengine wakifunga, kama akina Karim Benzema, huwa
hashangilii sana.

Comments