Guardiola huyoo Man City

 

Sasa ni rasmi kwamba kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola atajiunga

na Manchester City kiangazi kijacho.

Guardiola (45) atachukua nafasi ya Manuel Pellegrini (62) ambaye

amekiri kwamba ataondoka Etihad Juni 30.

Taarifa iliyotolewa na City imesema kwamba raia huyo wa City ‘aliunga

mkono kabisa’ hatua za kumchukua Guardiola.

Ikasema kwamba majadiliano yao na kocha huyo wa zamani wa Barcelona,

yalianza upya baada ya kukatika 2012, ambapo aliamua kwenda Bayern,

wakati huo Roberto Mancini akiwa kocha wa City na aliwapa ubingwa wa

England.

Pellegrini alichukua nafasi ya Mwitaliano huyo 2013 ambapo aliwapa

ubingwa wa England na Kombe la Ligi msimu uliofuata.

Ameshinda mechi 64 kati ya 99 za Ligi Kuu ya England akiwa kocha,

rekodi iliyovukwa na Jose Mourino tu aliyeshinda mechi 73 kati ya 99

za ligi hiyo akiwa bosi wa Chelsea.

City bado wana uwezo wa kutwaa mataji manne, idadi kubwa zaidi

inayowezekana, chini ya Pellegrini msimu huu.

Tayari wametinga fainali ya Kombe la Ligi, wanafukuzia nafasi ya

kwanza ya Ligi Kuu England, wamo kwenye michuano ya Kombe la FA na pia

katika hatua za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

City wanamchukua Guardiola, pengine kwa sababu ya kuwa kocha

aliyefanikiwa zaidi katika Barcelona, alikotwaa mataji 14 katika miaka

minne, ikiwa ni pamoja na ubingwa wa Hispania mara tatu na ubingwa wa

Ulaya mara mbili.

Pellegrini alichukua mapumziko ya mwaka mzima kabla ya kujiunga na

Bayern 2013, akisema alitaka kuinoa akili yake na kujiweka tayari kwa

kazi nzuri zaidi.

Huko nako ametwaa ubingwa wa Ujerumani mara mbili katika misimu miwili

na sasa anatafuta wa tatu, Bayern wakiongoza ligi kuu kwa pengo la

pointi nane.

Atapenda pia kutwaa ubingwa wa Ulaya na Wajerumani hao kabla ya

kuhamia England, ambako alipata kusema alikuwa na hamu ya kufanya

kazi, moja likiwa anataka kukaa kwenye jiji la Kiingereza kubadili

makazi.

Pellegrini analalamikiwa kwamba maendeleo ya klabu yamekuwa si

endelevu, timu ikiyumba nyakati fulani na kupoteza mechi

zisizotarajiwa.

Comments