Ujerumani wawapopoa Poland

Euro 2017

Ujerumani wamekwea kwenye uongozi wa Kundi D kwenye mechi za kufuzu kwa fainali za Euro 2016, baada ya kuwafunga Poland 3-1.

Yalikuwa mabao ya Thomas Muller aliyefunga kirahisi kwa mpira wa juu huku shujaa wao aliyewapa bao kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana, Mario Gotze akifunga mawili.

Poland walichomoa moja kupitia kwa Robert Lewandowski, bao lililokuja kabla ya lile la pili la Gotze, lililomwacha kipa wa zamani wa Arsenal, Lukasz Fabianski anayekipiga pia Swansea, akishindwa kuzuia.

Jamhuri ya Ireland, katika kundi hilo hilo, waliwafunga Gibraltar 4-0 huku Scotland wakilala 1-0 kwa Georgia. Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Ujerumani walilala kwa jirani zao wa Poland 2-0. Ujerumani, hata hivyo, wanaonekana kushuka kiwango uwanjani wakilinganishwa na walivyokuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Katika mechi nyingine, Ireland Kaskazini waliwafunga Visiwa vya Faroe 3-1, Finland wakawashinda Ugiriki 1-0, Hungary na Romania wakaenda suluhu sawa na ilivyokuwa kwa Denmark na Albania, huku Serbia wakiwaua Armenia kwa 2-0.

 

Comments