Kombe la Ligi ni hivi

*Tottenham Hotspur v Arsenal*

 

Ratiba ya michuano ya Kombe la Ligi imetolewa, ambapo mabingwa watetezi, Chelsea wataanza kazi kwa safari ya kwenda kucheza na Walsall walio kwenye League One.

 

Hii ni michuano ya tatu kwa ukubwa England na Wales, kwani mikubwa zaidi ni Ligi Kuu ya England (EPL) ambayo mabingwa ni Chelsea pia, ikifuatiwa na Kombe la FA linaloshikiliwa na Arsenal kwa msimu wapili mfululizo.

Ratiba kamili ya capital one...
Ratiba kamili ya capital one…

 

Katika raundi hii ya tatu ya Kombe la Ligi, Arsenal watakuwa wageni wa mahasimu wao wa London, Tottenham Hotspur wakati Aston Villa nao watakuwa wenyeji wa watani wao wa jadi jijini kwao, Birmingham City.

 

Manchester United watakuwa nyumbani kucheza na Ipswich Town huku Liverpool nao wakiwa nyumbani kucheza na Carlisle. Mechi hizi zitachezwa katika wikiendi inayoanzia Septemba 21.

 

Vigogo wengine wa EPL watakaokutana ni Sunderland watakaokuwa wenyeji wa Manchester City, Norwich wakiwakaribisha West Bromwich Albion huku West Ham wakisafiri kukwaana na Leicester.

advertisement
Advertisement

Comments